Home Michezo MASHINDANO TAIFA YA GOFU WATOTO YAFUNGWA TPC MOSHI KILIMANJARO WATOTO 45 WASHIRIKI

MASHINDANO TAIFA YA GOFU WATOTO YAFUNGWA TPC MOSHI KILIMANJARO WATOTO 45 WASHIRIKI

0

Mshindi wa jumla ibrahim shila wa tpc akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi mwenyekiti wa klabu ya lugalo brigedia jenerali michael luwongo (mstaafu) kwenye shindano la tanzania juniors open 2021 lililofanyika tpc moshi.

Mchezaji wa klabu ya lugalo karim rashid akipokea zawadi kutoka kwa nahodha wa klabu ya lugalo captain japhet masai mara baada ya kutangazwa mshindi division a wa shindano la tanzania juniors open 2021 lililofanyika tpc moshi.

Mchezaji shufaa twalib akipewa zawadi na rais wa chama cha gofu wanawake tanzania tlgu sophia vigo baada ya kutangazwa mshindi kama mchezaji pekee wa kike  kwenye shindano la tanzania juniors open 2021 lililofanyika tpc moshi.

Wachezaji watoto (juniors) kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kufunga shindano la tanzania juniors open 2021 lililofanyika tpc moshi. 

…………………………………………………………………………….

Mwenyekiti wa klabu ya golf ya lugalo brigedia jenerali mstaafu michael luwongo ameviomba vilabu vya golf nchini kuwekeza kwa watoto ili kuleta maendeleo ya kweli ya mchezo huo.

Ameyasema hayo wakati wa kufunga mashindano ya watoto yaliyofanyika kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2021 kwenye viwanja vya klabu ya gofu tpc iliyopo moshi kilimanjaro kaskazini mwa tanzania.

aidha brigedia jenerali mstaafu luwongo amewashukuru wazazi wa wachezaji hao kwani wameonyesha moyo wa dhati katika kuendeleza vipaji vya watoto hasa kwenye gofu.

luwongo aliongeza kwa kusema kuwa klabu ya lugalo ipo tayari kupeleka wachezaji sehemu yoyote ile kushiriki mashindano kwani ni moja na utalii wa ndani kwa watoto.

naye mratibu wa mashindano hayo klabu wenyeji jaffari ally amesema wamefarijika na ushiriki wa watoto hasa kutoka klabu ya lugalo kwani imekua ikijitahidi kutoa idadi kubwa ya wachezaji ukilinganisha na vilabu vingine

aidha jaffar ally amemshuku mwalimu wa watoto wa lugalo pro athumani chihundu kwani ameonyesha moyo wa dhati  kuwalea watoto na kukuza vipaji vyao huku akiwataka walimu wengine kuiga mfano huo.

‘‘niwashukuru sana walimu hasa mwalimu wa lugalo pro chiundu ana mapenzi kwa watoto na siku zote mwenye mapenzi kwa watoto huwa anaonyesha namna gani yupo karibu na watoto, kwahiyo walimu hata wa vilabu vingine igeni moyo huo,, alisema jaffar ally

kwa upande wa washindi mchezaji ibrahim shila wa  tpc ameibuka kinara kwa mikwaju 157  huku divisheni a mshindi ni karim rashidi aliyepiga mikwaju 165 na  divisheni b mshindi ni jamal juma aliyepiga mikwaju 148, wawili hao wakitokea lugalo huku shufaa twalibu mchezaji pekee wa kike kutoka lugalo akiibuka  na ushindi wa mikwaju 154 na hivyo kuwa mshindi pekee kwa wanawake.

mwenyekiti wa chama cha gofu tanzania tgu chris martin amesema shindano hilo la watoto (juniors) limeingizwa rasmi katika kalenda ya mashindano na hivyo shindano hilo litafanyika kila mwaka katika vilabu vitakavyochaguliwa.

kwa upande wake rais wa chama cha gofu wanawake taifa tlgu sophia vigo amesema tlgu inaunga mkono jitihaza hizo ambapo amesema watajitahidi kuongeza idadi ya wasichana ili kuleta ushindani katika mashindano mbalimbali.

‘‘tuna hakika mtaona wasichana wengi watakuja watashiriki kwenye haya mashindano kama tutakubaliana tgu na tlgu kwamba haya mashindano yanafanyika kila mwaka, na kuhakikisha  kama hivi wanavyosafiri kumleta na matron kwaajili ya kuwaangalia hawa vijana wetu wote’’