*********************************
Watendaji wa kuu wa Wakala wa Barabara kutoka nchi saba barani Afrika
walio chini ya wizara za Ujenzi wametakiwa kuwa na mifumo sahihi ya
taarifa za barabara itakayosaidia kuokoa fedha za Serikali ili
kutambua mahitaji mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya
barabara katika nchi zao kwa wakati unaofaa.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha mkuu wa wilaya ya
Longido, Frank Mwaisumbe katika mafunzo ya siku Saba yanayofanyika
jijini Arusha amezitaka taasisi hizo kuja na majawabu sahihi
yatakayoondoa changamoto kwenye Mtandao wa barabara katika nchi hizo.
Alisema kuwa pamoja na ujenzi ukarabati wa barabara zetu bado suala
la takwimu za ujenzi na ukarabati hazijawekwa kwenye mifumo ya
Kanzidata inaonyesha kutokuwepo hivyo kupoteza mapato ya serikali kwa
ucheleweshaji wa ujenzi kwa kukosa takwimu sahihi.
“Tanroads Tarura shirikianeni kwa pamoja katika kuanzisha kanzidata ya
pamoja itakayosaidia kuweza kukarabati kujenga barabara zetu ndani ya
muda unaohitajika na kuondoa changamoto katika mfumo wa taarifa za
barabara zetu za ndani kupata taarifa mapema na kuzitatua kabla
hazijaharibika utasaidia kuokoa fedha za Serikali”
Kwa upande wake Katibu mtendaji wa Shirikisho la barabara nchini Hagai
Bishanga Alieleza kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na
wizara ya ujenzi na Uchukuzi na kuzishirikisha nchi 7 ambazo ni
Msumbiji Tanzania Zimbabwe Siraleon Liberia Moroco Kenya na Uganda ili
kupata uzoefu na kuja na maazimio ya pamoja yatakayopeleke ujenzi wa
barabara nzuri za kimataifa.
alisema kuwa bado kumeendelea kuwa na changamoto kubwa ya kukosa
taarifa sahihi za mifumo ya ujenzi na ukarabati wa barabara zetu ili
kuchochea uchumi wa mataifa yetu ikiwemo kutokuwa na takwimu sahihi
ambazo mifumo ya utambuzi na sera zisizokidhi mahitaji
Akizungumzia changamoto kubwa katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya
barabara kuwa ni pamoja na fedha kidogo zinazotengwa ambazo hazikidhi
mahitaji , mfano hapa nchini ni fedha inayotengwa ni nusu ya mahitaji
yaliokusudiwa.
Alisema changamoto nyingine Ni kutokuwa na mifumo sahihi inayotoa
taarifa kuhusu matumizi ya barabara bila kuathiri matumizi ya barabara
pamoja na sera zilizopo hazikidhi mahitaji.