Home Mchanganyiko KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI

0

***************************

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, imetembelea na kukagua Mradi wa nyumba za makazi ya askari na baadae ikatoa mapendekezo kwa serikali kuona namna bora ya nyumba hizo kuweza kutumiwa na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamisi Chilo amesema kamati imependekeza na kushauri kuanza kutumika kwa nyumba za Polisi zilizopo Kunduchi, Mikocheni na Oysterbay ambapo nyumba hizo zitasaidia kupunguza changamoto za makazi kwa askari wa Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa, ziara ya kamati hiyo imetoa mwanga kwa Jeshi hilo na kwamba yeye na watendaji wake wamejipanga na kwamba wanasubiri kuruhusiwa ili askari Polisi waweze kuzitumia nyumba hizo.