Home Mchanganyiko WAJASIRIAMALI ANZENI KUTUMIA MISIMBOMILIA KWENYE BIDHAA MNAZOZALISHA ILI KUYAFIKIA MASOKO YA...

WAJASIRIAMALI ANZENI KUTUMIA MISIMBOMILIA KWENYE BIDHAA MNAZOZALISHA ILI KUYAFIKIA MASOKO YA KIMATAIFA-DKT.KIHAMIA

0

*****************************

Na Ahmed Mamoud Arusha

Wajasiriamali Kote nchini wameaswa kujiunga program ya Msimbomilia
(Barcorde)unaotambulika kimataifa utakaowasaidia bidhaa zao
kutambulika kwenye masoko ya kimataifa ya ndani na njee ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Dkt.Athman
Kihamia wakati akizindua mpango wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo
wajasiriamali na wafanyabiashara wa mkoa huo juu ya umuhimu na
matumizi ya msimbomilia Barcordes na ufuatiliaji wa mfumo wa
ufuatiliki na viwango yaliondaliwa na kampuni ya Global Standard one
(GS1) iliyofanyika jijini Arusha.

Alisema kuwa alama hizi za mistari yaani Msimbomilia ni muhimu sana
kwenye Mnyororo wa Ugavi ambao unahusisha wazalishaji wa bidhaa kwenye
kubadilishana taarifa kwa bidhaa kwani zisizo na Barcorde zinakosa
sifa ya kuingia kwenye Mnyororo wa Ugavi hivyo kumsababishia
mzalishaji kutofikia viwango hivyo kupungua kwa mauzo yake sokoni.

Dkt.Kihamia alisisitiza kuwa uzalishaji unaoenda sambamba na matumizi
bora ya Tehama utasaidia kuongeza ubora wa bidhaa zetu zinazozalishwa
na wakulima hapa nchini hivyo kusaidia kuingia kwenye masoko ya
kimataifa ya ndani na njee ya nchi na kufikia kwenye maendeleo ya
kweli yatakayosaidia kuongeza uzalishaji wenye tija.

“Wajasiriamali nendeni mkasome Sido na Veta kwa lengo la kuongeza
mnyororo wa thamani wa bidhaa zenu ili kupata usajili wa Tbs bure na
serikali yenu imeona umuhimu huo wa kupata huduma za msimbomilia kwa
bei ya offer utakaongeza uzalishaji wenye ubora kwenye masoko ya
kimataifa ya ndani na nje ya nchi”

Aidha kutokana na serikali kuona changamoto hizo kwa maksudi na nia
thabiti ya kuisaidia jamii ya wajasiriamali,wafanyabiashara na sekta
binafsi iliamua kushiriki mchakato wa kuanzishwa kwa taasisi ya
ufuatiliaji katika bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi
uanachama katika shirika la GS1 Global ambalo lina hatimiliki ya
huduma kadhaa ikiwemo Msimbomilia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Masoko wa kampuni ya GS1  hapa nchini Eric
Kafula alisema kuwa katika kusherehekea miaka kumi ya shirika hilo wao
na serikali kupitia Tamisemi wameandaa mafunzo hayo kwa mikoa 10 hapa
nchini juu ya umuhimu wa kuwa na Misimbomilia kwenye bidhaa za
wajasiriamali na mkoa wa Arusha umepewa kipaumbele baada ya kugundua
ni mji wa kitalii una fursa nyini za kibiashara na wengi wanahitaji
kuwa na masoki ya uhakika.

Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 barani Afrika ambazo
bidhaa zao zinatumia huduma ya Misimbomilia na hivyo kuongeza utambuzi
wa ubora wa bidhaa zake kwenye masoko ya kimataifa na kuwataka
wajasiriamali kwenda kusoma Sido na Veta ili waweze kupata nembo ya
TBS bure kwani gharama za usajili kwa wajasiriamali ni kubwa hivyo
watumie fursa hiyo ya serikali yetu.

“Kwenye mafunzo ya kusherehekea miaka 10 ya kuanzishwa Taasisi yetu ya
GS1 tumetoa offer ya ujisajili wa huduma ya Misimbomilia kwa nusu bei
kwa wajasiriamali wote watakaoshiriki mafunzo yetu kwani pamoja na
bidhaa nyingi kuzalishwa na kukosa utambuzi wa mifumo ya kimataifa ya
Tehama lakini pia kulikuwa na changamoto katika uchumi wa nchi kwa
wazalishaji wengi na wafungashaju kushindwa kupata huduma hii kwenye
bidhaa zao “

Nae Meneja wa Sido mkoani Hapa Nina Nchimbi alisema serikali kwa kuona
umuhimu wa uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ndio maana wakaja na
mafunzo maalum yanayotolewa na taasisi zetu za Sido na veta ili
wajasiriamali waweze kupata nembo ya TBS bure ndani ya miaka mitatu
kuanzia sasa.

“Niwaombe ndugu zangu wajasiriamali tumieni fursa hii ya kuongeza
ubora wa bidhaa zenu kuja kupata Elimu na mafunzo ya uzalishaji wenye
tija kwetu utakaosaidia kupata TBS bure na hivyo kuongeza mnyororo wa
Ugavi na kuyafikia masoko ya kimataifa”