Home Mchanganyiko UN KUSAIDIA UTEKELEZAJI MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA NCHINI

UN KUSAIDIA UTEKELEZAJI MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA NCHINI

0

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milizic, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milizic,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la UN katika maonyesho ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milizic, amesema Siku ya Mazingira Duniani ilianzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha wadau wa mazingira kujadili namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Bw.Milizic amesema hayo leo June 5,2021 jijini Dodoma  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo amesema Dunia inakabiliwa na hatari ya mabadiliko ya mazingira kutokana na uharibu wa mazingira.

“Changamoto nyingi zinazoikumba dunia kwa sasa ni matokeo ya uharibifu wa ardhi, maji na mazingira,” ameeleza Bw.Milizic

Hata hivyo amesema UN itasaidia kuharakisha utekelezaji wa mkakati utunzaji mazingira nchini ambao umelenga kuhuisha mfumo ikolojia nchini pamoja na mapitio ya sera ya mazingira

“Shirika litaendelea kuwa mdau wa mstari wa mbele kuwezesha shughuli za utunzaji mazingira nchini na tayari tuna miradi ya kurejesha mifumo ya ikolojia na tutaendelea kushirikiana kukabiliana na changamoto ya taka za plastiki,”amesema .

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya, amesema  shirika hilo litaendelea kuwa mdau wa mstari wa mbele kuwezesha shughuli za utunzaji mazingira nchini.

“Tayari tuna miradi ya kurejesha mifumo ya ikolojia na tutaendelea kushirikiana kukabiliana na changamoto ya taka za plastiki,” Clara amesema.