Menejimenti ya Infinix wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua simu mpya ya kwanza aina ya Infinix NOTE 10 Pro yenye uwezo mkubwa kuliko simu za Infinix
Afisa Mahusiano Infinix Bi. Aisha Karupa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Infinix NOTE 10 Pro uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Simu mpya ya kwanza ya Infinix NOTE 10 Pro.
Msanii wa Bongo Fleva Bw. Joseph Haule (Professor Jay) akicheza muziki na mke wake, katika hafla ya uzinduzi Infinix NOTE 10 Pro ni alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima.
Msanii wa kike maarufu kutoka lebo ya WCB Zuchu akitoa burudani ya muziki katika hafla ya uzinduzi wa Infinix NOTE 10 Pro.
Kiongozi Infinix akitoa historia fupi ya kampuni tangu kuanzishwa kwake nchini Hong Kong na hadi ilivyoingia rasmi Tanzania mwaka 2018 na kuelezwa malengo ya Infinix kwa wananchi wa Tanzania kwa miaka ijayo.
*****************************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kampuni ya simu Infinix imezindua simu mpya ya kwanza aina Infinix NOTE 10 Pro yenye sifa ya kuwa na G95 processor, RAM GB 8, ROM 128 yenye uwezo wa kufanya shughuli zote za kiofisi kwa haraka na ufanisi ikiwemo kukaa na chaji kwa muda wa masaa 11 uku ukisikiliza muziki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa simu ya Infinix NOTE 10 Pro, Afisa Mahusiano Infinix Bi. Aisha Karupa, amesema kuwa ni simu ya kwanza yenye processor kubwa zaidi kuliko simu yoyote ambazo waliwai kutoa awali.
“Infinix NOTE 10 Pro inauwezo mkubwa, inafanya kazi kwa ufanisi na inaweza kukaa na chaji muda mrefu, hivyo ni rafiki pia katika maeneo yenye changamoto ya ukosefu wa umeme” amesema Bi. Karupa.
Bi. Karupa amesema kuwa Infinix NOTE 10 pro ni simu ambayo imekuwa ikizungumziwa kwa muda mrefu mitandaoni na watu wengi kuwa na shahuku kutaka kutumia ambapo inatumia kamera nne za nyuma zinavyochukua picha kwa pamoja zikiongwozwa na kamera kuu ya MP64.
Simu ya Infinix NOTE 10 pro imepewa heshima ya namna yake ambayo itakuwa inauzwa na makupuni ya mawasiliano Tigo na Vodacom Plc na mteja kupewa ofa ya kutumia huduma ya internet mwaka mmoja bure.
Uzinduzi huo ulianza kwa kutoa historia fupi ya kampuni tangu kuanzishwa kwake nchini Hong Kong na hadi ilivyoingia rasmi Tanzania mwaka 2018 na kuelezwa malengo ya Infinix kwa wananchi wa Tanzania kwa miaka ijayo.
Wadau mbalimbali walishiriki akiwemo Joseph Haule (Professor Jay) na wasanii wa kizazi kipya walipata fursa ya kushereheshwa akiwemo msanii wa kike maarufu kutoka lebo ya WCB Zuchu pomoja na wakali wa dance kutoka Jsquare.