Home Mchanganyiko WANANCHI WA MAFIA WAPATA HUDUMA ZA MADAKTAR BINGWA KUTOKA JAMII BORA

WANANCHI WA MAFIA WAPATA HUDUMA ZA MADAKTAR BINGWA KUTOKA JAMII BORA

0

Mtaalam wa Afya kutoka Jamii Bora Dr Hanifa  akitoa malekezo kwa wanachi waliofika kupata huduma 

Sehemu ya wananchi wa Kisiwa cha Mafia wakisubiri Kuonana na Madaktari Bingwa kutoka Mtandao wa Jamii Bora

****************************************************************

MBUNGE wa Jimbo la Mafia Mkoani Pwani ambae pia  NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Omary Kipanga ameupongeza Uongozi wa matandao wa Wataalam  wa Afya wa jamii bora kwa kuwezesha wananchi wa jimbo hilo kupata matibabu bure kutoka kwa madaktari Bingwa

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Huyo, katika Ufunguzi wa kambi ya siku mbili ya matibabu bure kutoka madaktari Bingwa wa Mtandao wa JamiiBora ya Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mafia Juma Salum amesema kuwa ni jambo la faraja kwa wananchi kupata huduma hiyo

 Aidha ametoa wito  kwa wadau wengine wa afya kuiga mfano huo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wemekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mtandao wa Jamiibora Dakta Abbas Mussa amesema lengo la kufanya hivyo ni kutekeleze malengo ya mtandao huo la kuhakikisha jamii inapata huduma kutoka kwa madaktari bingwa katika maeneo yao  ambayo yamekuwa hayafikiwi na wataalam hao

Aidha amesema kuwa katika mtandao huo kuna madaktari bingwa wa aina mbalimbali ikiwemo macho,afya ya akili,magonjwa ya akina mama na watoto pamoja na magonjwa mengine ambapo wataalam hao wa afya takribani 45 watakuwa kisiwani Mafia kwa lengo la kuwahudumia wananchi bure

Nae Amiri wa Jumuiya ya JAI Yahya Masao ameitaka jamii kuwa na muamko katika kuchangia damu kwa lengo la kusaidia makundi yenye uhitaji.

Wananchi wa Kisiwa cha Mafia wametoa shukrani zao kwa Mtandao wa wataalam wa Afya  Jamii Bora kwa huduma hizo ambapo zimewasaidia kutokusafiri hadi Jijini Dar es salaam ili kuonana na Madkari hao bingwa