Home Michezo SIMBA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA 3-1 NAMUNGO MECH YA LIGI KUU

SIMBA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA 3-1 NAMUNGO MECH YA LIGI KUU

0

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba wametoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Namungo FC mchezo uliopigwa uwanja wa Majaliwa Ruangwa Mkoani Lindi.

Namungo walienda mapumziko wakiwa na bao moja lililofungwa na Kiungo Mshambuliaji Styve Nzigamasabo dakika ya 22.

Kipindi cha pili Simba timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo wageni walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 78 Chriss Mugalu aliisawazishia Simba bao.

Mabao mengine ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 83 akipokea pasi ya Chriss Mugalu na dakika ya 87 Bernard Morrison aliwanyanyua mashabiki wa Simba akifunga bao kwa shuti la mbali.