Home Mchanganyiko STAMICO YASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UZINDUZI WA KITABU CHA MWONGOZO UWEKEZAJI MKOA WA...

STAMICO YASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UZINDUZI WA KITABU CHA MWONGOZO UWEKEZAJI MKOA WA MARA

0

********************

Leo tarehe 28 Mei 2021 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki kikamilifu katika shughuli ya uzinduzi wa Kitabu cha Mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Mara. Shughuli hii imefanyika leo na Mgeni rasmi katika tukio hili alikuwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Pamoja na ushiriki wa uziduzi huu wa kitabu cha Mwongozo wa uwekezaji, STAMICO pamoja na Tume ya Madini na wadau kutoka sekta binafsi walishiriki kwa pamoja kuwaelimisha wananchi wa Mkoa wa Mara shughuli mbali mbali kupitia maonesho yaliyofanyika kwa jumla ya siku tatu mfululizo viwanja vya shule ya Msingi ya Mukendo.