Home Mchanganyiko WAHITIMU WAMETAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO KUJENGA FURSA

WAHITIMU WAMETAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO KUJENGA FURSA

0

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Rais Mstaafu wa awamu ya nne) Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akiwatunuku vyeti wahitimu katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wahitmu wakiwa kwenye maandamano katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Rais Mstaafu wa awamu ya nne) Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akiwa katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wahitimu wakiwa katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Jaji Mstaafu Mhe.Damian Lubuva akizungumza katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye akizungumza katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Wahitimu Chuo kikuu cha Dar es Salaam,wametakiwa kutumia taaluma na ujuzi wao kutafuta fursa ili kuweza kujiajiri na si kusubiri kuajiriwa.

Ameyasema hayo leo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye katika mahafali ya 51 kwa minajili ya kutunuku digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada na astashahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

kizungumza katika mahafali hayo, Prof.Anangisye amewahasa  wahitimu kutafuta furs abadala ya kusubiri fursa ziwafuate ambapo ni jambo si rahisi kutokea katika ulimwengu wa sasa.

“Msisubiri kuajiriwa na  serikali bali kuweni wepesi kuangalia ni wapi ujuzi wenu unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi hata kama itabidi ufanye kazi za kujitolea”. Amesema Prof.Anangisye.

Aidha Prof.Anangisye amewataka wahitimu ambao wanarudi kwenye vituo vyao vya kazi kwenda kuongeza tija katika majukumu yao na kuzingatia kanuni kuu za uadilifu katika kuwatumikia watanzania.

Pamoja na hayo Prof.Anangisye amesema wataendelea kumuenzi na kumkumbuka Hayati Dkt,John Pombe Magufuli kwa yale ambayo ameyafanya katika chuo hicho ikiwemo kusimamia ujenzi wa nyumba za kukaa wanafunzi maalufu kama Magufuli hosteli na kuchochea miundombinu katika chuo hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho Jaji Mstaafu Mhe.Damian Lubuva amewasihi wahitimu hao  kuwa werevu katika kuzikabili changamoto za maisha watakazokumbana nazo.

“Fanyeni bidii kutafuta fursa za kuendeleza maihsa.Tunawaasa muwe na ushirikiano na umoja katika kila mnayoyafanya kwa kuwa karibu na jamaa na jamii zenu kwa ujumla ili muendelee kunufaika na upendo utokanao na jamii”. Amesema Mhe.Lubuva.