Home Mchanganyiko TAKUKURU DODOMA KUENDELEA KUMCHUNGUZA ALIYEFANYA UDANGANYIFU WA MILIONI 58

TAKUKURU DODOMA KUENDELEA KUMCHUNGUZA ALIYEFANYA UDANGANYIFU WA MILIONI 58

0

………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mkoani Dodoma,  inaendelea na uchunguzi dhidi ya Mtuhumiwa Lyato Bihemo Mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa kufanya udanganyifu na kulipwa Sh. milioni 58.3 na kampuni ya Vodacom na HTT Infranco LTD.

Fedha hizo amelipwa kama malipo ya kukodisha eneo la kuweka mnara wakati eneo hilo ni msitu wa hifadhi wa Isabe uliopo Halmashauri ya Kondoa mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema kuwa uchunguzi umebaini fedha hizo zilipaswa kulipwa kwa serikali ya kijiji au Halmashauri.

Amefafanua kuwa uchunguzi umeonyesha kwamba mtuhumiwa huyo alisaini mkataba wa ukodishaji wa eneo hilo na Vodacom 2009, kwa kipindi cha miaka 10 na kujifanya mmiliki halali wa eneo hilo.

Hata hivyo Bw.Kibwengo amesema  sekta ya ardhi kinara wa vitendo vya rushwa kwa asilimia 15 ya malalamiko yaliyopokelewa na taasisi hiyo tangu Julai 2019 hadi sasa.

Bw.Kibwengo amesema kuwa  wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia utendaji wa mabaraza ya ardhi ya kata kwamba yamekuwa ya utendaji unaoashiria vitendo vya rushwa.

Amesema kuwa TAKUKURU imefanya juhudi mbalimbali za kuondoa rushwa,ikiwemo kuchambua mifumo ya utendaji wa mabaraza hayo na kuyashauri kuondokana na hali hiyo.