Home Michezo KASEKE AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP YAICHAPA...

KASEKE AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP YAICHAPA 2-0 MWADUI FC

0
Timu ya  Yanga SC wamefanikiwa kutinga  Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mabao yote ya Yanga yamefungwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke dakika ya 25 na 57 na kwa ushindi huo, Yanga SC watakutana na Biashara United,Nusu Fainali hiyo itachezwa  katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi 
Robo Fainali za michuano hiyo,  zitachezwa kesho kati ya Rhino Rangers na Azam FC hapo hapo Kambarage majira ya saa kumi jioni  na usiku Simba SC ma Dodoma Jiji FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.