***************************
Katika tukio la kwanza,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. STEVEN ADAM MWAKAMYANDA [40] Mkazi wa Bagamoyo – Tukuyu na 2. NURU WILLIAM TAMSON [28] Mkazi wa Igogwe – Tukuyu wakiwa na mali za wizi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 22.05.2021 majira ya saa 03:00 usiku huko Mtaa wa Igogwe, Kata ya Kawetele, Tarafa ya Tukuyu mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya wakiwa na mali za wizi ambazo ni:-
Spedi 14,
Misumali ya bati viloba 21/2,
Mfuko 01 wenye misumali ya kenchi inchi 4,
Cement mfuko 01 wa Tembo fast,
Kamba za manila 16,
Mitungi ya gas 02,
TV 01 inchi 24 aina ya zola na remote zake,
Deki 02 na remote zake,
Redio Subwoofer 2 aina ya Sundar na Aborder zikiwa na speaker zake,
Flash Disk 05,
Pikipiki T-Better nyekundu haina plate namba,
Waya wa umeme mita 061/2,
Pesa kichele [silver] jumla Tshs 218,200/= na
Mabati 6 gauge 30 yenye urefu wa mita 3.
Mali zote hizo zimetambuliwa na mhanga.
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. JUSTINE AUGUSTINO [24] Mkazi wa Ilalabwe – Tukuyu na 2. MPOKI BELMAN [26], Dereva Bajaji na Mkazi wa Ilomba Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na mali za wizi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 23.05.2021 majira ya saa 11:00 asubuhi huko maeneo ya Kijiji cha Idweli, Kata ya Usongole, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya wakiwa na mali za wizi Redio 01 Subwoofer aina ya Pinetech na Spika zake tatu [03] zikiwa zimepakiwa kwenye Bajaji MC 352 BPT TVS. Mali zote zimetambuliwa na mhanga alievunjiwa nyumba yake usiku na kuibiwa.
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MALEWA BEKI @ HUSSEIN [24] Mkazi wa Itumbi – Chunya kwa tuhuma za kupatikana na mali ya wizi Ng’ombe 06.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.05.2021 majira ya saa 15:00 alasiri huko Kitongoji cha Kisalasi, Kijiji na Kata ya Mamba, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya akiwa na Ng’ombe hao ambao tayari wametambuliwa na mhanga aitwaye JOHN GIMBUI.
Ng’ombe hao waliibwa huko Kijiji cha Iseche – Mkwajuni, Wilaya ya Songwe, Mkoa wa Songwe nyumbani kwa mhanga