Home Michezo SIMBA SC YAINYUKA 3-0 KAIZER CHIEFS, YAONDOLEWA KWENYE MICHUANO KWA MABAO 3-4

SIMBA SC YAINYUKA 3-0 KAIZER CHIEFS, YAONDOLEWA KWENYE MICHUANO KWA MABAO 3-4

0

**************************

NA EMMANUEL  MBATILO

Klabu ya Simba Sc imeishindwa kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya Kaizer Chiefs ya nchini Afika Kusini katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Simba imepata magoli hayo katika uwanja wa Benjamini Mkapa hivyo kufanya matokeo kuwa 3-4 Kaizer Chiefs  kupata faida kwa mabao aliyofunga katika hatua ya kwanza walipokutana.

Mabao ya Simba Sc yalifungwa na mshambuliaji John Bocco ambaye alifunga mabao mawili katika dakika ya 24 na 56 ya mchezo na goli la tatu liliwekwa kimyani na kiungo mshambuliaji raia wa Zambia Clautos Chama dakika ya 86 ya mchezo.

Simba Sc sasa iatelekeza nguvu zake katika ligi kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la FA.