Home Burudani DOGO JANJA AZINDUA RASMI ALBUM YA ‘ASANTE MAMA’

DOGO JANJA AZINDUA RASMI ALBUM YA ‘ASANTE MAMA’

0

*********************

Dar es Salaam, 21 Mei 2021; – NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Abdulaaziz Chende almaarufu ‘Dogo Janja’ ameachia albamu yake iliyobeba jina la ‘Asante Mama’, ikiwa ni albamu yake ya pili baada ya ile ya kwanza iliyofahamika kama ‘Mtoto wa Uswazi’.

Albamu ya ‘Asante Mama’ imebeba nyimbo kumi na moja ambapo kati ya nyimbo hizo, tisa amewashirikisha wanawake tu. Nyimbo zinazopatikana kwenye albamu hii ni pamoja na ‘Intro’, ‘Feel Aje’ ft Rosa Ree, ‘Mama’ ft Khadija Kopa, ‘Asante’ ft Lady Jay Dee, ‘Polepole’ ft Linah, Umenishinda ft Lulu Diva, ‘Mziki’ ft Maua Sama, ‘Shundulia Chini’ ft Mimi Mars, ‘Nuru’ ft Nandy, ‘Mayo’ft Patricia Hillary na My life Remix ft Radio & Weasel.

Albamu hii itapatikana kwenye App ya Boomplay tu kwa muda wa wiki mbili ambapo mashabiki wataweza kusikiliza na kupakua nyimbo zote tisa buree.

Akiizungumizia albumu hiyo, Msanii Dogo Janja amesema ilikua ndoto yake kufanya kazi na wanawake tu ili kuonyesha thamani waliyonayo katika maisha yake na amefurahi kuona ndoto hiyo ikitimia .

“Ndoto ya kuja na albamu ambayo imeshirikisha wanawake tu ni kutokana na malezi ya Mama ambaye kwangu ni nguzo bora maishani. Hivyo, kwangu hii ni kama zawadi kwa wanawake wote na nina furaha iliyopitiliza kutimiza ndoto hii”.

‘Albamu ya Asante Mama imetayarishwa katika studio mbili, Upward Music chini ya Genius & 66 na MJ Records chini ya Daxo Chali na Marco Chali kwa ushirikiano wa karibu na Kampuni ya Boomplay na Dogo Janja mwenyewe, hivyo naamini wapenzi wa muziki wangu watafurahia kazi zangu hizi mpya,” alimalizia kusema Dogo Janja.