Home Michezo NIC WADHAMIN DAR CITY MARATHON

NIC WADHAMIN DAR CITY MARATHON

0

**********************************

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limedhamini mbio za Dar City Marathon zinazotarajiwa  kufanyika  tarehe 23 mwezi Mei mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukuza vipaji vya michezo nchini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo ndugu Yessaya Mwakifulefule amesema licha ya kuwa michezo ni furaha, michezo ni ajira kwa vijana, hivyo, kupitia mbio hizo wana imani ipo siku vijana wenye vipaji watapata ajira.

Aidha waandaji wa Dar City Marathon wamelishukuru Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa.

Katika hatua nyingine Katibu wa Riadha Taifa Bi Ombeni Zavara amelipongeza Shirika la Bima la Taifa kwa ushirikiano wa hali na mali linaoutoa katika sekta ya michezo na kutoa rai kwa mashirika mengine kuiga mfano wa NIC katika kudhamini mbio,kwani ndiyo sehemu pekee ambapo wanariadha wa kitafa hupatikana.