Home Siasa MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP ISDOR MPANGO AFUNGA KAMPENI ZA UBUNGE BUHIGWE

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP ISDOR MPANGO AFUNGA KAMPENI ZA UBUNGE BUHIGWE

0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Buhigwe Wilayani Buhigwe MKoani  Kigoma Mhe. Felix  Kavejuru kwenye Mkutano wa ufungaji wa  Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo  wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 16 Mei 22021, kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Philip Isdor Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ufungaji wa Mkutano huo umefanyika leo Mei 15,2021 katika Uwanja wa Muyama Buhigwe Kigoma.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akijumuika pamoja na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Buhigwe kucheza ngoma za CCM alipowasili katika Uwanja wa Muyama Jimbo la buhigwe Mkoani Kigoma kwa ajili ya ufungaji  wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Buhigwe kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa kiti cha Ubunge unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 16 Mei 2021, kutokana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Philip Isdor Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania