Home Mchanganyiko WANANCHI LUDEWA MBIONI KUKUA KIUCHUMI

WANANCHI LUDEWA MBIONI KUKUA KIUCHUMI

0

************************

Ofisi ya mbunge jimbo la Ludewa Joseph Kamonga imeanzisha programu ya kutoa elimu kwa wananchi wilayani Ludewa iliyopewa jina la KAMPENI YA UCHUMI iliyolenga kuwaelimisha wananchi hao kutambua fursa zilizopo kata kata zao na wilaya kwa ujumla pamoja njia ya kuzitumia fursa hizo ambayo tayari yameanzakwa baadhi ya kata na yanatarajiwa kuwafikia wananchi katika kata zote 26 za wilaya hiyo.

Program hiyo ambayo itafanyika kwa awamu kwa kipindi cha miaka miwili yamelenga kuelimisha jamii na vikundi mbalimbali ili kuweza kuzitumia fursa hizo kama fursa za kilimo, uvuvi na nyinginezo za kimkakati na kukuza uchumi ambapo mpaka sasa tayari wamekwishatoa elimu katka kata ya Manda, Luhuhu, Ludewa, masasi, Mundindi,Luilo pamoja na Mavanga .

Akizungumza katika mikutano ya kutoa elimu hiyo iliyofanyika katika baadhi ya kata katibu wa mbunge huyo Alphonce Mwapinga amesema ofisi ya mbunge inatambua umuhimu wa wananchi wake katika kukua kiuchumi hivyo ikaona itoe fursa hiyo kwa wanchi ili waweze kupata elimu kwa kuwaleta mtaalamu wa uchumi ili awape darasa .

Amesema elimu hiyo inayotolewa itawasaidia wananchi kukuza maendeleo yao binafsi kiuchumi na wilaya kwa ujumla na wanaamini kwa kupitia vikundi hivyo wanavyowapa elimu wanaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“ofisi ya mbunge inatambua kwamba vikundi vinafaida kubwa, na ukitaka kumuwezesha mwananchi awe na uchumi mzuri ni lazima apate elimu ya kuendana na mazingara ya hali ya uchumi iliyopo hivyo tunaamini tukitoa elimu kwa kikundi cha watu 30 au zaidi tunaimani itafika nbali kwakuwa watawaelimisha na wenzao”, Alisema Mwapinga.

Aliongeza kwa kuwatangazia neema wananchi wanaoishi katikakata za mwambao mwa ziwa nyasa hasa wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi kuwa mbunge wao Joseph Kamonga anawapambania bungeni ili katika ukanda huo kuweze kuanzishwa vizimba ndani ya ziwa nyasa vya ufugaji wa samaki ili ziwa hilo liweze kutoa samaki wengi zaidi kama maziwa mengine na kukuza uchumi kupitia sekta ya uvuvi.

Aidha kwa upande wa mtaalam wa uchumi Lucia Mwaipopo amesema anamshukuru mbunge huyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya kutoa elimu kwa wananchi wake ambapo kwa sasa ameanza kwa kuvitambua vikundi mbalimbali na mahitaji yake pamoja na fursa zilizopo katika kata hizo.

Amesema programu hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miaka miwili ambapo kila eneo litaelimishwa kulingana na fursa zilizopo huku akitumia mfano wa kilimo cha mihogo kwa ukanda wa mwambao ambao hulima sana kilimo hicho kuwa kutokana na msaada wa mbegu walizopewa na mbunge wao wanapaswa kuzitumia kwa tija kamba ambavo wanavyotumia wenzao wa Butihama ambako mbegu hizo zilitoka.

Ameongeza kuwa wanapaswa kujadili mikakati yao ya kukuza zao hilo kupitia mbegu bora walizopata kwa kuona kwa jinsi gani watafanya biashara kama ni kwa kuuza mihogo yenyewe au kutengeneza bidhaa za chakula zinazptokana na mihogo hiyo.

“Kila jambo linapaswa kufanywa kwa malengo, hutuwezi kutumia mbegu bora kwa kilimo cha mazoea wakati wenzetu wanakuza uchumi wao kupitia mbegu hizo hizo za mihogo, tunapaswa kulima kilimo cha kisasa na chenye tija na maslahi kiuchumi”, Alisema Mwaipopo.

Hata hivyo kwa upande wa madiwani wa kata mbalimbali wamemshukuru mbunge Kamonga kwa proghamu hiyo adhimu sana, huku wananchi wao wakifurahia fursa hiyo na kusema kuwa itawasaidia katika kufanya shughuli zao za kiuchumi kulingana na dunia inavyokwenda.

Theresia Nyando ni mmoja wa wananchi hao amesema yeye anavikundi viwili ambavyo vinashughulika na kuweka akiba na kukopa hivyo kwa elimu hiyo wanayopata itakuwa na faida kwao kwani wataweza kujitanua zaidi katika shughuli za kiuchumi badala ya kuishia kuweka fedha na kukopa