Home Biashara WAZIRI BASHUNGWA ASISITIZA TAASISI YA HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI TANZANIA (COSOTA) KUONGEZA KASI...

WAZIRI BASHUNGWA ASISITIZA TAASISI YA HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI TANZANIA (COSOTA) KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MIRAHABA NA KUTOA GAWIO

0

…………………………………………………………………..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa   ameisisitiza Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki  Tanzania  (COSOTA) kuongeza kasi katika ukusanyaji wa Mirabaha na kujipanga kutoa gawio  kwa Wasanii katika mwaka mpya wa fedha wa 2021/22.

Mhe.Bashungwa ametoa maagizk hayo leo Mei 11,2021 alipofanya ziara katika  Ofisi za Taasisi hiyo, Bodi ya Filamu pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  zilizopo katika Majengo ya Utumishi, Kivukoni Dar es Salaam.

Taasisi hizo zipo katika jengo moja  kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wa Sekta ya Sanaa nchini