Home Uncategorized WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WANAOTOKA JIMBO LA KISESA WATINGA BUNGENI MWALIKO WA...

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WANAOTOKA JIMBO LA KISESA WATINGA BUNGENI MWALIKO WA MH. LUHAGA MPINA

0
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina

Viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa
katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja
vya Bunge jijini Dodoma na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina

Baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa ndani ya ukumbi
wa Bunge  wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto


Sehemu ya baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakifuatilia mjadala
wa hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto bungeni Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk. Doroth Gwajima mara baada ya kuwasilisha hotuba yake bungeni
Dodoma.
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanaotoka Jimbo
la Kisesa wamefika bungeni kujifunza namna Bunge linavyoendesha shughuli
zake huku wakiahidi kusoma kwa bidii ili waweze kutoa mchango
unaostahili kwa jimbo lao na Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti
wa Umoja wa wanafunzi wa vyuo  kutoka Jimbo la Kisesa, Ndugu Sitta
Kuzenza Nyangwakwa amesema umoja huo umeanzishwa kwa lengo la
kuwakutanisha pamoja vijana wote wanaosoma vyuo mbalimbali kuanzia ngazi
ya Diploma hadi Digrii wanaotoka Jimbo la KIsesa.
Amesema
tayari wanafunzi wa vyuo wanaotoka Jimbo la Kisesa  kutoka Mikoa ya
Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya  wanaendelea kujiunga ili kuunga
mkono juhudi za  Serikali pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
katika kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo huku akitumia nafasi hiyo
kuwahamasisha vijana wengine wanaotoka Jimbo la Kisesa kujiunga na umoja
huo.