…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Manyara
Katika ziara zake mhe RAHHI amejadili changamoto mbalimbali za kina mama na namna ya kwenda kuzitatua.
Moja ya changamoto kubwa aliyokutana nayo ni uhaba wa maji na amesema kuwa maeneo mengi ya Mkoa wa Manyara yana uhaba wa maji hivyo yeye kama mwakilishi wa kina mama amelichukua tatizo hilo na kulipeleka Bungeni tayari kwa kwenda kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Vilevile Mbunge huyo amewaasa kina mama kusimamia elimu ya mtoto wa kike na amesema ili mtoto wa kike aweze kutimiza ndoto zake ni lazima asimamiwe vizuri katika kupata elimu na hilo ni jukumu kubwa la kina mama na amesema ukimpa mwanamke elimu vizuri anakuja kuwa kiongozi bora, mchapakazi na mwadilifu.
Changamoto nyingine ya wanawake ni unyanyaswaji ambapo mhe Rahhi amekemea tabia ya baadhi ya wanaume kunyanyasa wanawake zao.
Mhe Mbunge pia amegusia suala la Afya na hili ameliasa kwenda kupigania kuongezwa kwa madawa katika hospital za Mkoa wa Manyara, pia ili kina mama waepukane na changamoto za huduma za kliniki ni lazima uboreshwaji wa huduma upatikane.
Pia amesema ili wakina mama waweze kujidhatiti kwenye ujasiriamali vizuri ni lazima huduma muhimu kama maji, elimu na afya wawe wamezipata vizuri huduma hizo.
Hata hivyo, Mbunge huyo amewaasa wanawake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi pendwa Ya Tanzania.