Home Michezo SIMBA NA YANGA ZAKWEPANA ROBO,NUSU FAINALI KOMBE LA FA

SIMBA NA YANGA ZAKWEPANA ROBO,NUSU FAINALI KOMBE LA FA

0

……………………………………………………………………

Droo ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Shirikisho (ASFC) baada ya kutoka imesababisha vigogo wa Soka nchni Simba na Yanga kukwepana hatua ya Robo Fainali na Nusu Fainali.

Yanga mwaka huu kuanzia 16 bora mechi zake zimekuwa za ugenini ambapo leo imepangwa kuanzia tena ugenini kucheza na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga.

Mabingwa wa Ligi Kuu Simba wao mechi zao zote watacheza nyumbabi watacheza na Dodoma Jiji Robo Fainali

Mechi za robo fainali zinatarajia kuanza kuchezea kati ya Mei 25 mpaka 27 mwaka huu.

Mechi za nusu fainali ambazo zitapigwa katika viwanja vya Maji maji Songea mkoani Ruvuma na Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Nusu fainali ya kwanza itazikutanisha msindi wa mechi ya Simba vs Dodoma na Rhino Rangers vs Azam FC huku nusu fainali ya pili itakutanisha mshindi wa mechi ya Biashara United vs Namungo na Mwadui vs Yanga.

Kwa Ratiba hiyo Simba na Yanga haziwezi kukutana katika hatua ya Robo Fainali pamoja na Nusu Fainali hivyo nafasi ya kukutana inaweza kuwa katika Fainali ya Michuano hiyo na Mshindi wa Kombe hilo atapata nafasi ya kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika