Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahan (wa tatu walio kaa kutoka kushoto) akiwa na Vijana wa Kikundi cha Jitume Vijana Ikungi.baada ya kutembelea mradi wa ufyatuaji matofali wilayani humo jana.
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahan (wa pili walio kaa kutoka kushoto) akiwa na Vijana wa Puma Youth Group.baada ya kutembelea mradi wa ufyatuaji matofa wilayani humo jana.
Vijana wakipakia matofali kuzipeleka eneo la ujenzi wa nyumba tano za watumishi.
.
Na Dotto Mwaibale, Singida
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka vijana waliokopa asilimia 4 kutoka Halmshauri zote za Mkoa wa Singida kuwa waaminifu kwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Ndahani alitoa ombi hilo jana wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya vikundi vya vijana wilayani Ikungi.
Akizingumuza katika kikundi cha Vijana cha Puma kilichopo wilayani Ikungi alisema
vijana wengi wanajuwa kuwa fedha za halmshauri ni ruzuku au sadaka ,nataka mtambue kuwa fedha hizo ni mkopo ambao kwa upendo wa Serikali umeweka masharti nafuu hivyo ninawataka vijana kurejesha fedha mlizokopa kulingana na mkataba uliowekwa ili zikawasaidie vijana wengine ambao hawajapata.
Aidha Ndahani amewakumbusha wanavikundi kutunza kumbumbuku za biashara zao na kuwa waaminifu wao kwa wao.
Alisema vikundi vingi havitunzi kumbumbuku jambo ambalo linasababisha kushindwa kudhibiti mapato na matumizi ya fedha zao ikiwemo usomaji wa taarifa za vikundi.
Ndahani amewahakikishia vijana wa Mkoa wa Singida kuwa Serikali ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iko bega Kwa bega kuhakikisha vijana wanawezeshwa kiuchumi ili kuondokana na umaskini hivyo vijana wanapaswa kuanzisha vikundi na kuvisajili katika maeneo yao.
Aidha Serikali ya sita inaendelea kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme ambao utasaidia vijana kuanzisha miradi mbalimbali vikiwemo viwanda vidogo vidogo na vya kati.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Peter Mussa alisema wanaendelea kuwapatia vikundi vya vijana, wanawake na walemavu elimu ya ujasiriamali sanjari na kuwawezeshaji kiuchumi.