Home Uncategorized DC DKT.SERERA ATAMBUA MCHANGO WA WANAHABARI DODOMA”CPC YATOA TUZO KWA WADAU

DC DKT.SERERA ATAMBUA MCHANGO WA WANAHABARI DODOMA”CPC YATOA TUZO KWA WADAU

0

MKUU wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Dkt.Seleman

Serera  amesema  tasnia ya Habari ina mchango mkubwa katika

kuibua changamoto za jamii ili kuweza kutatuliwa na serikali.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha hayo leo leo

8,2021  katika maadhimisho ya uhuru wa

vyombo vya Habari mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya  Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma (CPC) kwa

kushirikiana na Umoja wa  Klabu za

Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA)pamoja

na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA).

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma

Dkt.Binilith Mahenge ,mkuu huyo wa wilaya amesema vyombo vya habari vimekuwa na

mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi 

huku pia akiwataka wanahabari kuendelea kuwa na ubunifu katika

uchakataji wa habari .

Vyombo vya habari vinatoa hamasa kubwa katika

maendeleo ya nchi.Waandishi mmeibua changamoto nyingi ambazo nyingine sisi

viongozi hatuwezi kuziona.Lakini mnavyozionesha mnatupa fursa sisi kuzitatua na

kuboresha maisha ya wananchi.


Dkt.Seleman Serera 

Katika hatua nyingine  amewataka wanahabari kuendana na mabadiliko ya

sayansi na teknolojia na kuhakikisha wanaandika habari zenye mizania (balance)

ili kuweza kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Mwenyekiti wa CPC Musa Yusuph akitoa neno

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari mkoa

wa  Dodoma (CPC) Musa Yusuph ameainisha

changamoto zilizopo katika tasnia ya  

habari ikiwemo mialiko isiyozingatia uzito wa matukio ya kihabari.

Mwenyekiti huyo amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wadau wa habari ambao wamekuwa wakitoa mialiko kwa vyombo vichache vya habari huku wakijua jambo hilo ni nyeti na linahitajika kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Tuwaombe wenzetu mnaoratibu matukio au habari za viongozi wa Umma,habari hizo kila mwandishi anazihitaji hivyo unapoalika vyombo vichache ni kuwanyima Watanzania haki yao kupashwa habari.

Mussa Yusuph

Naye Katibu

Mkuu wa Klabu hiyo Ben Bago amewasihi baadhi ya Wadau wa Habari kuacha tabia ya  kutoa lugha isiyokuwa na

staha kwa wanahabari pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Katibu huyo amebainisha kwamba baadhi ya wadau wamekuwa kwenye migongano ya mara kwa mara na waandishi kutoka na kauli za kejeli na dharau zinazotolewa.

Malalamiko mengi tunayopokea ni kuhusu baadhi ya wadau kuwatolea lugha zisizo na staha kwa waandishi,tujifunze kuvumiliana na tutambue wote lengo letu ni kufikisha taaluma kwa umma


Ben Bago

Afisa Mhifadhi mkuu Mamlaka ya Hifadhi Tanzania
(TANAPA) Jully Lyimo akitoa mada

Afisa Mhifadhi mkuu Mamlaka ya Hifadhi Tanzania

(TANAPA) Jully Lyimo pamoja afisa utalii mkoa wa Manyara Cecilia Nkwabi

wamelezea mchango wa Habari katika sekta ya utalii nchini ambapo wamesema  waandishi wa habari na Sekta ya utalii ni

kama mapacha hivyo wanasaidiana katika kazi.

Pia TANAPA imetoa Wito kwa Watanzania kutembelea

hifadhi za taifa ili kujifunza mambo mbalimbali huku wakibainisha kuwa mamlaka

hiyo ipo mbioni kuanzisha Utalii wa Michezo (sports Tourism).

Sanjari na hilo CPC imetoa tuzo kwa wadau mbalimbali

ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa watu na taasisi ambazo zinachangia

ustawi wa tasnia ya habari katika mkoa wa Dodoma.

Mgeni rasmi Dkt.Seleman Serera (katikati) akimkabidhi tuzo Afisa Mhifadhi mkuu
Mamlaka ya Hifadhi Tanzania (TANAPA) Jully Lyimo

 

Mgeni rasmi Dkt.Seleman Serera (katikati) akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya
Maji na Usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) Bw.Sebastian Warioba 

Tuzo hizi ni endelevu,tunahitaji kuona ushirikiano

kati ya Waandishi na Wadau wa Habari unaimarika,hivyo kila mwaka tutatoa tuzo

ili kuwatambua wale wanaowezesha wanahabari kufanya kazi katika mazingira

rafiki. 

Ben Bago.

Katika tuzo TANAPA na DUWASA walipokea tuzo kwa

upande wa taasisi zenye mchango mkubwa kwa waandishi wa habari,huku Afisa

Uhusiano wa TANESCO mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza akipokea tuzo ya Afisa

Habari bora wa mwaka.

Lupenza ameibuka mshindi baada ya kuwashinda

wapinzani wake wa karibu Catherine Sungura (Wizara ya Afya) na Everlyn Thomas

(Ofisi ya CAG).

Mapendekezo ya majina na kura hizo zilipigwa na

Wanachama wa CPC ilikumpata mshindi ambaye vigezo vikuu ni ushirikiano (kufikika,kauli

nzuri na Msaada kwa waandishi) kwa Waandishi wakati wanatimiza majukumu yao.

Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo

Pia Sebastian Warioba amepata tuzo ya mwanachama bora wa CPC kwa mwaka 2020-2021.Warioba ametunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo ya makao makuu ya nchi.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani kitaifa

yalifanyika Mei 3, 2021  Jijini Arusha

ambapo mkoa wa Dodoma yamefanyika Mei,8,2021 yakienda sambamba na kaulimbiu

isemayo Habari kwa Manufaa ya Umma .