Home Mchanganyiko WAZIRI NDALICHAKO AZITAKA TAASISI ZINAZOIBUA BUNIFU KUONGEZA KASI,AZINDUA KILELE CHA MASHINDANO YA...

WAZIRI NDALICHAKO AZITAKA TAASISI ZINAZOIBUA BUNIFU KUONGEZA KASI,AZINDUA KILELE CHA MASHINDANO YA MAKISATU

0

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akikagua mabanda wakati wa uzinduzi wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza wakati akizindua  kilele cha Mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akisisitiza jambo wakati akizindua kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

  

Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,(hayupo pichani) wakati wa akizindua kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akizindua  kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Akwilapo,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

  

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua  kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yaliyoanza leo Mei 7,2021  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako amezitaka taasisi zote zinazohusika na kuibua bunifu za teknolojia hapa nchini kuongeza kasi katika kuzitambua bunifu mpya katika ngazi mbalimbali ili kama nchi tuweze kujenga uwezo wetu wa ndani bila kutegemea teknolojia za nje.

Waziri Prof. Joyce Ndalichako ameyabainisha hayo leo may 7, 2021 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Amesema lazima taasisi zote zinazohusika na uibuaji wa bunifu za teknolojia lazima ziongeze kasi ya kuziibua na kuziendelea bunifu hizo ili katika kuwezesha mapinduzi ya kiteknolojia katika sekta mbalimbali zikiwamo afya na kilimo.

“Natambua kuna mwongozo wa kuwatambua wabunifu katika halmashauri zetu kwahiyo nawaelekeza msimamie kuhakikisha mwongozo ule unafanya kazi kwa sababu naamini tunao wabunifu wengi sana kuliko wale tunaowaibua kupitia MAKISATU” amesema Prof. Ndalichako.

Amesema serikali inatambua umuhimu wa ubunifu wa teknolojia hapa nchini na kwa kutambua wabunifu kukosa sehemu za kufanyia kazi zao serikali imeanzisha vituo atamizi 17 nchini kwa lengo la kulea ubunifu wa teknolojia mbalimbali zilizowezesha kuanzishwa kwa kampuni 94 zilizoweza kutoa ajira 600 kwa watanzania.

Pia amesema wameanzisha kumbi za ubunifu katika vyuo mbalimbali vikiwamo chuo kikuu cha Dar es saalam na Dodoma na taasisi ya sayansi ya Karume vyote ni kuhakikisha wanapanua wigo wa watanzania kuendeleza ubunifu wao ili uweze kuleta tija.

Amesema serikali imewekeza kuanzia ngazi ya chini kabisa ili kusaidia kutambulika na kuendeleza vipaji vya watoto na kujenga jamii yenye misingi imara ya ubunifu tangu wakiwa na umri mdogo.

“Nimepita katika mabanda mbalimbali kwa kweli nimeona bunifu za watoto wadogo wa shule za msingi kwakweli kwa umri wao ni hatua kubwa sana” amesema.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu mbalimbali hapa nchini na kutaka wabunufu wajitokeze zaidi, ambapo kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH serikali imetoa zaidi ya bilioni 3.2 ili kuwezesha bunifu mbalimbali zinazobuniwa.

Pia amesema serikali imefanya marekebisho katika mitaala ya kufundishia teknolojia za kidigitali imeanzishwa kwenye taasisi za elimu ya juu ili ziwezeshe kupatikana kwa wabunifu wengi wanaopita katika vyuo hivyo.

Amesema kwa miaka mitano kutoka 2015 hadi 2020 wametambua wameendeleza taknolojia mbalimbali na miradi 215 imefadhiliwa na serikali katika kuhakikisha kuwa bunifu zinaibuliwa na kuleta manufaa kwa watanzania.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Akwilapo, amesema mashindano hayo yalianzishwa mwaka 2019 na ni moja ya mikakati ya wizara ya kuibua na kutambua ubunifu wa teknolojia zinazovumbuliwa na watanzania.

Amesema katika kipindi cha miaka miwili jumla ya wabunifu 1066 wameibuliwa na kutambuliwa na Wizara, na wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Wizara ambapo wanasimamiwa na taasisi mbalimbali.

“Bunifu 26 kati ya 130 zipo katika hatua ya kubiasharisha katika sekta mbalimbali, pia 83 zinaendelea kuboreshwa ili kufikia kwenye kubiasharishwa, na 21 zipo katika hatua ya awali kuelekea kuboreshwa.” Amesema.

Ameongeza kuwa kwa mwaka huu “Wabunifu 714 wamejitokeza kushiriki katika makundi saba ambapo lengo ni kupata wabunifu 70, mchujo ulikuwa mkali sana, wabunifu hawa watashindanishwa kupitia tathmini itakayofanywa na majaji na tutapata wabunifu 21 ambao watatambuliwa na kupewa zawadi zao siku tutakayokuwa tunahitimisha,”amesema.

Amesema taasisi 50 zinashiriki katika maonesho hayo ikiwamo wabunifu 24 walioshiriki mwaka 2019 na 2020 na wengi wao ni wale ambao bunifu zao zinaendelezwa na serikali na zipo katika hatua mbalimbali.

Amesema maonyesho hayo yameanza leo may 7 na yanatarajiwa kuhitimishwa May 11, 2021 na yanashirikisha makundi saba ambao ni Shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi stadi, vyuo vya kati, nyuo vikuu, taasisi za utafiti na wabunifu kutoka mfumo usio rasmi.