Home Mchanganyiko SERIKALI YAAHIDI KUONDOA CHAMNGAMOTO ZINAZOWAKABILI MAKANDARASI.

SERIKALI YAAHIDI KUONDOA CHAMNGAMOTO ZINAZOWAKABILI MAKANDARASI.

0

Naibu waziri wa wizara  ya ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunga mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi.

Msajili wa bodi ya makandarasi  mhandisi Rhoben Nkori akiongea na waandishi wa habari juu ya matarajio yao baada ya kufungwa kwa mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi mwaka 2021.

***********************

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Naibu waziri wa wiraza ya ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara amesema kuwa serikali ipo tayari kuondoa changamoto zinazowakabili wakandarasi ikiwemo kuendelea kuwapa miradi isiyodhidi thamani ya bilioni 10 kwani wanaamini wana uwezo wa kuzifanya.
Waitara ameyasema hayo wakati wa akifunga mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi wa mwaka 2021 uliofanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa tumekubaliana kuwaendeleza makandarasi ndani kufanya miradi mikubwa.
“Tatawapa miradi na sio kwasababu hatupendi wageni lakini tunataka muwe na wivu na mali za Tanzania ili zianze kuwanufaisha nyie ndipo zikawanufaishe na wengine tunataka mnapojenga miradi muwe wazalendo kwani mkianza nyie na wengine watafuata,”Alisema Waitara.
Alisema kuna miradi mizuri iliyofanywa na wataalamu watanzania na imeonyesha uwezo mkubwa lakini pamoja na hayo aliwataka kwenda kutembelea mradi wa Kilosa na kumwambia  mkandarasi husila mapungufu yaliyopo katika mradi huo.
“Mkawaambie wanachokifanya kinawapotezea makandarasi wengine fursa ya kupewa miradi lakini pia nataka mfanye tathimini ya kitaalamu kuonyesha mapungufu yaliyopo katika miradi iliyotelelezwa kwa kutumia Force akaunti na mtakachokipendekeza ilimradi kiwe ndani ya uwezo wa serikali tutakifanyia kazi na kukiboresha,” Alieleza.
Kwa upande wake msajili wa bodi ya makandarasi  mhandisi Rhoben Nkori, alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kuangalia jinsi ya kuweza kuwawezesha  makandarasi kupata miradi ambapo zipo changamoto walizozieleza lakini kikubwa ni matumizi ya Force akaunti.
Mhandisi Nkori  alieleza kuwa ni matarajio yao kuwa serikali itatekeleza ahadi walizozitoa kwani wana imani nayo na wanajua kuwa kauli ya serikali ni kauli thabiti hivyo watapata miradi.
Naye mmoja wa makandarasi hao Zefania Kwayu kutoka kampuni ya  Zekwa trading LTD  alisema kuwa wamefurahia semina hiyo ya kikanda lakini pia wamefurahishwa na jinsi ambavyo serikali imeonesha nia ya kuwasaidia na wanaamini watapata majibu.
Alieleza lipo suala la wakandarasi kuchelewesha miradi lakini  lina mambo mengi mojawapo ikiwa ni uwezeshwaji wao kuwa chini pamoja na malipo kucheleweshwa jambo ambalo linawafanya makandarasi kuingia katika madeni mengi  na ndiyo chanzo cha mradi kutokukamilika kwa wakati.