Home Mchanganyiko IKULU YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA INAYOSAMBAA RAIS MHE.SAMIA KUAGIZA KUACHIWA KWA WAFUNGWA...

IKULU YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA INAYOSAMBAA RAIS MHE.SAMIA KUAGIZA KUACHIWA KWA WAFUNGWA 23 WA KISIASA

0

**********************

NA EMMANUEL MBATILO

Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Ikulu, Mhe.Gerson Msigwa amewataka Watanzania kupuuza taarifa zilizorushwa na moja ya television kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu kuagiza wafungwa wa kisiasa nchini kuachiwa huru.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Mhe.Msigwa amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote na Mheshimiwa Rais hawezi kuingilia uhuru wa mahakama.

“Mheshimiwa Rais hajazungumza kitu chochote kuhusiana na wafungwa wa kisiasa, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa”. Amesema Mhe Msigwa.

Aidha Mhe.Msigwa amesema kuwa kupitia crip inayosambaa kueleza taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Mheshimiwa Rais amemuagiza mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaachia hao wafungwa 23 ambao hawapo.

“Mheshimiwa Rais aingilii uhuru wa mahakama pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali aendeshi masuala kama haya ya mahakamani kwa mujibu wa sheria zetu na taratibu zetu hivyo Watanzania wapuuze taarifa hizo hazina ukweli wowote”. Amesema Mhe.Msigwa.

Pamoja na hayo Mhe.Msigwa amesema mpaka sasa Serikali imeanza kuchukua hatua na ofisi yetu ya ubalozi Nairobi inachukua hatua kufuatilia kwanini chombo hicho kimepotosha kiasi hicho.