Kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kimefanyika Arusha tarehe 6 Mei 2021.
Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kukamilisha agenda mbalimbali za msingi zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 Mei 2021.
Miongoni mwa Agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi ni pamoja na Taarifa ya Utafiti wa Kuboresha Mfumo na Muundo wa Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Rasilimali zilizopo pamoja na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaongozwa na Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Bi. Amina KH. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Ujumbe wa Burundi ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na uchumi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Ujumbe wa Uganda nao ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu |
Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu |
Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha Makatibu Wakuu |
Kikao kikiendelea |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Wajumbe wakifuatilia kikao |
Kikao kikiendelea |