Mkuu wa idara ya kemia Dkt. Juma Mongoyo kushoto
akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa NIMR Profesa Yunus Mgaya ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya sita ya utafiti katika chuo kikuu
kishiriki cha elimu Mkwawa “MUCE
Mtafiti Princess Ngowi kushoto akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa NIMR Profesa Yunus Mgaya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya sita ya utafiti katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa “MUCE.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WATAFITI kutoka chuo kikuu
kishiriki cha elimu Mkwawa “MUCE” cha mjini iringa wamegundua dawa ya kuzuia
sumu kuvu kwenye mazao ya nafaka inayotokana na mitishamba ugunduzi unaotajwa
kuleta suluhisho katika uhifadhi wa mazao hayo
Akizungungumza katika maonesho ya
sita ya utafiti dkt. Juma Mongoyo ambaye ni mkuu wa
idara wa kemia katika chou kikuu kishiriki cha mkwawa aliseama walifanya
utafiti kupitia mmea aina ya Diospyros Mafiensis ambao uligunduliwa Mafia
ambapo walitumia mizizi yake katika utafiti na kuleta matokeo chanya ya utafiti
huo
Mongoyo alisema kuwa katika
tafiti za mmea huo wamebaini kuwa mizizi yake hufanya kazi ya kupunguza uzalishaji wa sumu kuvu na
kulinda nafaka isishambuliwe na fangasi aina ya Asperigillus flavus na Asperigillus
parasiticus wanaozalisha sumu kuvu kutokana na joto kali na unyevunyevu
unaotengeneza fangasi hao.
Dkt. Mongoyo alisema kuwa takwimu zinaonesha
kuwa takribani ya watu million 4.5 duniani wanakula sumu kuvu kwa kiwango
tofautitofauti ambapo huchukua miaka 30 hadi kujitokeza madhara yake huku
akisema kuwa takwimu huonyesha takribani watu laki moja na elfu hamsini na tano
hupoteza Maisha kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo la saratani ya maini
inayosababishwa na ulaji wa sumu kuvu.
Alisema kuwa mizizi ya mmea huo
wa diospyros mafiensis unauwezo wa kulinda nafaka na jamii yote inayoweza
kushambuliwa na fangasi hao wajulikanao kama Asperigillus flavus na Asperigillus
parasiticus
Akizungumza mgeni rasmi katika uzinduzi huo
ambaye ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjjwa ya binadaamu “NIMR”
prof.Yunus Mgaya alisema kuwa taasisi ya NIMR imeona ipo haja ya kushirikiana
na chuo cha Mkwawa kutokana na tafiti
hizo wanazozifanya zina lengo moja na taasisi ya NIMR ya kulinda afya ya
binadamu
Alisema kuwa tafiti iliyofanyika
na chuo kikuu kishiriki cha Dar es salaam Mkwawa kuhusiana na mmea unaotumika
katika tiba asili ambayo wakatengeneza dawa yenye kemikali inayozuia fangasi isizalishe sumu ambayo ikiingia
kwenye mahindi yanayotumiwa na binadamu husababisha saratani ya ini hivyo
utafiti huo unaweza ukakinga jamii dhidi ya magonjwa yatokanayo na sumu kuvu.
Aidha profesa Yunus Mgaya
aliongeza kuwa katika kuboresha tiba nchini taasisi ya NIMR inajenga kiwanda
cha kuzalisha dawa za asili zitokanazo na mimea ambazo zitakuwa kwa mfumo wa
vidonge na unga tofuti na sasa hivi ambapo dawa nyingi za asili ni za maji.
Akizungumza naibu RASI taaluma wa
chuo cha mkwawa dkt. Evaristo Haulle alisema kuwa ushirikiano wa taasisi zote
za utafiti na za elimu ya juu kuwa na ushirikiano na asisi nyingine ni muhimu
hivyo wamepokea kwa mikono miwili ushirikiano kati ya mkwawa na nimr
Maonesho hayo ya utafiti
yanajumusha wanafunzi na waalimu watafiti kutoka chuo kikuu hicho kishiriki cha
elimu ikiwa ni maandalizi ya kwenda kushiriki maonesho ya wiki ya utafiti ya
chuo kikuu cha Dar es salaam yanayobeba kauli mbiu isemayo “utafiti na uvumbuzi
endelevu kwa maendeleo ya viwanda”