Home Mchanganyiko Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi akabithi mipira ya  maji kwa wananchi.

Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi akabithi mipira ya  maji kwa wananchi.

0
Mbunge wa Arumeru magharibi Noah Lemburis Saputu akimshika mkono Diwani wa kata ya Nduruma ,Raymond Mollel baada ya kukabithi mipira ya maji(rollas)kwa wananchi wa Kijiji cha Mzimuni ,walioko pembeni ni baadhi ya wananchi hao wakishuhudia tukio hilo.(Happy Lazaro)
***************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Noah Lemburis Saputu  amekabithi mipira ya maji (rollas)  kwa ajili ya  kutekeleza mradi wa maji zenye dhamani ya takribani shs 10 milioni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Aidha mipira hiyo imekabithiwa  katika Kijiji cha Mzimuni kilichopo kata ya Nduruma  na  kijiji cha Sasi kilichopo kata ya Bangata wilayani Arumeru .
Akizungumza wakati wa kukabithi mipira hiyo,Mbunge huyo amesema kuwa,vijiji hivyo vimekuwa vikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Maji kwa muda mrefu ambapo wananchi wake wamekuwa wakipata adha kubwa ya kuamka usiku kufuata maji umbali mrefu.
Amesema kuwa,mradi huo wa maji katika kijiji cha Mzimuni unatoka katika kata Mlangarini , ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa mipira hiyo kwa ajili ya kupeleka maji kijijini hapo.
“shughuli hii ya kuleta mipira katika vijiji hivi ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi zangu katika kampeni zangu baada ya wananchi kulalamikia changamoto ya upatikanaji wa Maji kwa muda mrefu katika vijiji hivi, na ndo kazi imeanza nitahakikisha natatua changamoto zote zinazowakabili wananchi wangu kwa kipindi Cha miaka mitano kwani ni miongoni mwa ahadi nilizozitoa kwao.”amesema Mbunge Noah.
Aidha  amewataka viongozi mbalimbali wa kata hiyo kushirikiana  na wananchi  na kuanza mara Mona shughuli  ya kutandaza mipira hayo ili wananchi wapate maji kwa haraka na kuondokana na adha hiyo.
Diwani wa kata ya Nduruma ,Raymond Mollel amesema kuwa,wanamshukuru Sana Mbunge kwa kuwaletea mipira hiyo ya maji kwani kwa Sasa changamoto ya maji katika Kijiji hicho itakuwa imeisha kabisa.
Mollel amesema kuwa,mradi huo wa Maji utawanufaisha wananchi zaidi  ya elfu nne kutoka Kijiji hicho Cha Mzimuni ambao walikuwa wakipata adha hiyo kwa maji mrefu Sana.
Nao baadhi ya wananchi wakizungumzia mradi huo,Saiguran Mollel amesema kuwa,anashukuru Sana kwa kitendo Cha Mbunge wao kuanza kutimiza ahadi alizotoa katika kata hiyo ikiwemo kutatua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wa muda mrefu .
“Tunamshukuru Sana Mbunge wetu kwa kutuletea hii mipira ya kusambaza maji kwani tulikuwa tunapata adha kubwa Sana ya kutembea umbali wa kilometa 5 kufuata huduma ya maji na  wakati mwingine ilitulazimu kutumia maji ya mfereji kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo,kwa kweli tupo tayari Sasa kuanza kuchimba mitaro kwa ajili ya kulaza  mipira tupate maji kwa haraka.”amesema .