Home Mchanganyiko MBUNGE CHIKOTA AISHAURI SERIKALI KUBORESHA MFUMO WA ELIMU NCHINI

MBUNGE CHIKOTA AISHAURI SERIKALI KUBORESHA MFUMO WA ELIMU NCHINI

0

…………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mbunge wa Nanyamba(CCM), Abdallah Chikota,ameishauri serikali kuboresha mfumo wa elimu nchini ili uweze kuleta matokeo chanya kwa wahitimu pindi wanapomaliza na kule wanapokwenda.

Ushauri huo ameutoa leo Mei 5,2021  bungeni jijini Dodoma akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika mwaka wa fedha 2021/22.

Mhe.Chikota amesema kuwa lazima kuwepo na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa elimu kwenye mabadiliko ya mitaala, sheria za elimu, walimu na wakufunzi kuandaliwa kabla ya kwenda kufundisha na kurudisha muundo wa zamani wa kumwezesha kamishna wa elimu kusimamia sekta zote za elimu badala ya maeneo machache.

Aidha ameeleza kuwa  serikali imekusudia kupitia sera ya elimu ya mwaka 2014, sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 hivyo kuipongeza kwakuwa inaenda vizuri manaa lazima yafanyike mabadiliko ya jumla si vipande vipande.

“Natilia mkazo kwenye mabadiliko ya mitaala na ni kweli kwamba sasa hivi kilio kingi kwa wana jamii kwamba wahitimu katika mfumo wetu wa elimu wanashindwa kukidhi haja ya mahitaji ya kule wanapokwenda,”amesema Mhe.Chikota

Ameioba Serikali kuwa wakati kazi ya maboresho ikifanya  shughuli hiyo uwepo  ushirikishwaji wa makundi yote wakiwemo walimu, jamii, wanafunzi, taasisi mbaimbali zinazohusika na masuala ya alimu wakiwemo wadau ili isiwe suala la wizara ya elimu peke yake.

“Tukishabadilisha mtaala sio kwamba tumefanikiwa kuna kazi kubwa inabidi ifanyike maana kuna kawaida ya kubadilisha mtaala bila kuangalia tunakwendaji katika kutekeleza,”amesema.

Chikota ameeleza kuwa tukishaandaa mtaala mpya uendane na mazingira ya shule na vyuo vyetu kutekeleza mtaala huo.