Home Mchanganyiko ATCL YASITISHA SAFARI ZA MUMBAI – INDIA  KUANZIA 4 MEI 2021 

ATCL YASITISHA SAFARI ZA MUMBAI – INDIA  KUANZIA 4 MEI 2021 

0

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), inapenda kuutaarifu umma na wateja wake wote kwamba imesitisha safari zake za ndege kati ya Dar es Salaam (Tanzania) na Mumbai (India) kuanzia 4 Mei, 2021 hadi hapo tutakapotoa taarifa nyingine ya kurudisha safari hizo. Hii ni kunatokana kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa COVID-19 nchini India. 

Aidha, abiria wote wenye tiketi za ATCL katika safari tajwa hapo juu wanashauriwa kuwasiliana na ofisi za ATCL au mawakala wao kwa taratibu za kubadilisha tiketi ili zitumike pindi safari zitakaporejeshwa tena bila gharama yoyote. 

Tunawaomba radhi wateja wetu wote kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0800110045.