Home Mchanganyiko PROF.NONGA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

PROF.NONGA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

0

Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga, akizungumza wakati akifungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifatilia hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga, wakati akifungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga,kumsikiliza mtoa mada katika mafunzo hayo Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Garvin Kweka,akitoa elimu za upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga,akiwaongoza watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupima afya zao mara baada ya kufungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakipima afya zao mara baada ya kupata  mafunzo pamoja na upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Mratibu wa Ukimwi, Vvu na magonjwa sungu yasiyoambukiza mahala pa kazi Sekta ya Mifugo Rachel Maliselo,akielezea mafunzo hayo waliopataiwa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo yameendana na  upimaji wa afya iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

Mtoa mada katika mafunzo hayo Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Garvin Kweka,akizungumzia lengo la mafunzo hayo ni kuongea na watumishi ili kuwasaidia kujenga tabia ya kutambua afya zao mara kwa mara iliyofanyika leo April 30,2021 Mtumba jijini Dodoma.

………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga,ametoa wito kwa  watumishi wa umma kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua afya zao kama ambavyo muongozo wa kudhibiti virusi vya ukimwi (Vvu),Ukimwi na magonjwa sugu yasiyo ambukiza mahala pa kazi unavyowataka.

Wito huo ameutoa leo April 30,2021 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo Prof. Hezron Nonga, wakati akifungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya kwa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Prof. Nonga amesema kuwa upimaji wa afya kwa watumishi wa umma kwa mujibu wa muongozo huo wa mwaka 2014 ni jambo la lazima siyo hiyari.

“Kupima afya ni jambo la lazima na muhimu sana kwa mtumishi kwani itasaidia hata kuongeza tija katika taasisi baada ya kutambua afya yake”amesema Prof.Nonga

Aidha amesema kuwa kwa kutambua afya za wafanyakazi kutamwezesha  mwajiri kuongeza ufanisi katika utekelzaji wa jukumu mbalimbali.

“Kama mtumishi atakuwa na afya njema basi atasaidia kuongeza uzalishaji katika taasisi hivyo wafanyakazi wanatakiwa kupima afya zao kwa mujibu wa muongozo huo wa kudhibiti vvu, ukimwi, pamoja na magonjwa sugu yasiyoambukiza”amesisitiza Prof. Nonga

Prof. Nonga amesema kuwa kwa mtumishi ambaye atabainika mara baadaya vipimo kuwa anamaambukizi ya virusi vya ukimwi taratibu zionamtaka mwajiri wake kumpatia kiasi cha Sh. 100,000 kila mwezi.

Prof.Nonga amesema kuwa mafunzo hayo kwa wafanyakazi pia watapatiwa mada mbalimbali kutoka kwa watalaam wa masula ya afya.

“Wafanyakazi watakiwa pia kufanya mazoezi ili kuondokana na tatizo la uzoto ulipiliza pamoja na msongo wa mawazo”amesema

Kwa upande wake mtoa mada katika mafunzo hayo Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Garvin Kweka, amesema  lengo la mafunzo hayo ni kuongea na watumishi ili kuwasaidia kujenga tabia ya kutambua afya zao mara kwa mara.

“Leo nimekuja kuzungumza na watumishi hawa kwani tumekuwa tukipoteza nguvu kazi nyingi kutokana na magonjwa, asilimia 60 ya watumishi inaonyesha wana tatizo la uzito kupindukia pamoja na msongo wa mawazo kwahiyo mafunzo haya yatawasaidi kutambua nini wafanye na kipi wasifanye ili kuwa na afya njema ili kuendelea kuleta tija katika maeneo yao ya kazi”amesema Dk.Kweka

Naye Mratibu wa Ukimwi, Vvu na magonjwa sungu yasiyoambukiza mahala pa kazi Sekta ya Mifugo Rachel Maliselo, amesema kuwa  lengo la zoezi hilo ni kutoa fursa kwa wafanyakazi kupima afya zao kwa mujibu wa muongozo huo.

“Wafanyakazi wetu wamefurahi sana kupata fursa hii kwani inawapa nafasi ya kutambua afya zao na kufanya kazai zao kwa bidii na kuongeza tija katika maeneo yaoa ya kazi”amesema Maliselo