Home Mchanganyiko KATIBU TSC AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI UKEREWE

KATIBU TSC AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI UKEREWE

0

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama akisaini daftari la wageni katika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Ukerewe wakati wa ziara yake iliyofanyika Aprili 30, 2021.

Mkurugenzi Ajira, Maadili na Maadili ya Walimu wa TSC, Christina Hape akisaini daftari la wageni katika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Ukerewe wakati wa ziara ya Katibu wa Tume iliyofanyika Aprili 30, 2021.

Katibu wa TSC Paulina Nkwama (wa pili kutoka upande wa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Ajira, Maadili na Maadili ya Walimu wa TSC, Christina Hape (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Msaidizi Maadili na Nidhamu, Robert Lwikolea (wa kwanza kulia) pamoja na mtumishi wa TSC Wilaya ya  Ukerewe, Magreth David (wa pili kutoka kushoto) wakati wa ziara ya Katibu wa Tume iliyofanyika Aprili 30, 2021.

*********************************

Na Adili Mhina.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama leo Aprili 30, 2021 amefanya ziara wilayani Ukerewe na kuwataka watumishi wa Tume hiyo kuhakikisha wanazingatia mwongozo uliotolewa na Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kushughulikia upandishaji wa madaraja ya walimu ili kuhakikisha haki inatendeka katika zoezi hilo.

Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Mkurugenzi wa Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu, Christina Hape pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Maadili na Nidhamu, Robert Lwikolela, Bi Nkwama alisema kuwa TSC imedhamiria kuondoa kero za walimu, hivyo watumishi ni lazima watumishi wa TSC wazingatie taratibu zilizowekwa na kujiepusha na masuala ya upendeleo wakati wa kutoa huduma kwa walimu.

Vilevile, Nkwama aliwataka watumishi wa TSC wilayani hapo kufanya ziara mashuleni kwa lengo la kutoa elimu kwa walimu juu ya msuala ya Ajira, Maadili na Maendeleo yao ili walimu waweze kuwa na uelewa mpana juu ya wajibu na haki zao katika utumishi wa Umma.

Aliongeza kuwa kuwafikia walimu mara kwa mara na kuwapa elimu kunasaidia walimu kujiepusha na makosa ya kinidhamu ambayo baadhi yao wanayafanya kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya sheria kanuni na taratibu za utumishi wa walimu.

Alisisitiza kuwa kwa kuwa TSC haina vyombo vya usafiri vya kutosha katika ofisi za wilaya, watumishi wa wilayani wanapaswa kuwa na ushirikiano wa karibu na ofisi za Halmashauri, kufanya kazi kama timu moja na kufanya ziara pamoja na watumishi wa sekta ya elimu wa Halmashauri badala ya kukaa na kulalamika kuwa wanashindwa kufanya kazi kwa kuwa hawana vyombo vyo usafiri.