Home Biashara KIKOSI CHA 837 KJ CHITA KUANZA MRADI MKUBWA WA UFUGAJI SAMAKI AINA...

KIKOSI CHA 837 KJ CHITA KUANZA MRADI MKUBWA WA UFUGAJI SAMAKI AINA YA SATO

0

 Kaimu kamanda Kikosi cha 837 KJ Chita  Meja Evergreen Bartazal,akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuanza  mradi mkubwa wa ufugaji wa samaki aina Sato walipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi hilo  katika kikosi cha 837 KJ Chita Leo April 22,2021 wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. 

Mtaalam wa Samaki kutoka Kikosi cha 837 KJ Chita Luteni Joseph Lyakurwa,akielezea ramani ya mchoro wa Bwawa la Samaki ambalo linatarajia kuanza  mradi mkubwa wa ufugaji wa samaki aina Sato walipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi hilo  katika kikosi cha 837 KJ Chita Leo April 22,2021 wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. 

Bwana Shamba Msaidizi Kikosi cha 837 KJ Chita Woz Joseph Mlingwa,akizungumza kuhusu ufugaji wa samaki aina Sato utakavyoanza  Leo April 22,2021 wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. 

kijana wa kujitolea katika Kikosi cha 837 KJ Chita William Lubinza,akielezea faida walivyoipata mara baada kujifunza katika Jeshi hilo huku akiehidi wataenda kuwa mabalozi Leo April 22,2021 wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. 

Muonekano wa Shamba la Mpunga lenye ekari 25000 lililopo katika Kikosi cha 837 KJ Kilichopo leo April 22,2021

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Kilombero

Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) linatarajia kuanza mradi mkubwa wa ufugaji wa samaki aina Sato ambapo wanatarajia kuanza uzalishaji wa mbegu za vifaranga vya samaki utakaosaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora za vifaranga vya samaki katika Kikosi cha 837 KJ kilichopo Chita Mkoani Morogoro 

Hayo yamebainishwa Chita,Wilayani Kilombero  Mkoani Morogoro Leo April 22,2021 na Kaimu kamanda Kikosi hicho Meja Evergreen Bartazal wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea katika kikosi hicho kuona mradi huo, amesema mradi huo utasaidia kutatua changamoto ya vifaranga kwa maana ya kujitosheleza shamba la Chita pamoja na mashamba mengine ya nje ya kikosi hicho.

“Tunashukuru mradi huu unaendelea vizuri tunatarajia utaleta matokeo chanya kwa jamii kwa sababu unakwenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbegu za vifaranga vya samaki, “amesema Meja Bartazal.

Amesema katika mradi huo kama ungetumia mkandarasi kutoka nje ya jeshi ulitarajiwa kugharimu sh milioni 440, lakini kwa kutumia wataalamu wa ndani ya jeshi hilo na vijana unatarajia kugharimu sh milion 250 katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake Mtaalam wa Samaki kutoka jeshi hilo Luteni Joseph Lyakurwa amebainisha kuwa kikosi hicho wana matangi 27 ambayo hutumika katika kilimo cha umwagiliaji pamoja na ufugaji wa samaki. 

Pia Luteni Lyakurwa amesema  matanki hayo yana uwezo wa kuzalisha tani 12 za samaki aina ya sato kwa mwezi  na vifaranga 200,000 ambavyo vitatumika katika kumaliza tatizo la uhaba wa mbegu bora za Samaki katika kikosi hicho. 

Luteni Lyakurwa amebainisha kuwa katika  Bwawa litakalojengwa  litakuwa kubwa kuliko mabwawa mengine hapa nchini ambalo  litasaidia kuongeza upatikanaji wa samaki,kutokana na hilo bwawa  linakwenda kumaliza tatizo la uhaba wa vifaranga bora vya samaki. 

Ameongeza kuwa “Mfumo huu wa uzalishaji vifaranga vya samaki kupitia mabwawa yanayojengwa  kwa sababu idadi ya watu inaongezeka kushinda vyanzo vya asili vilivyopo,” amesema.

Amesema baada ya bwawa hili kukamilika kati ya mabwawa ya nchi kavu litakuwa bwawa kubwa nchini ambapo kwa sasa lililopo linazalisha tani nne kwa mwezi.

Naye kijana wa kujitolea wa katika jeshi hilo William Lubinza amesema amepata elimu kubwa ambapo atakarudi uraiani ataitumia kujipatia kipato bila kutegemea ajira rasmi atakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine ambao hawajapata bahati ya kushiriki katika mafunzo ya Jeshi la kujenga taifa.