Home Mchanganyiko DED KIRASAWE AWAFUNDA WALIMU NA WANAFUNZI KUWA NA NIDHAMU ILI KUBORESHA KIWANGO...

DED KIRASAWE AWAFUNDA WALIMU NA WANAFUNZI KUWA NA NIDHAMU ILI KUBORESHA KIWANGO CHA ELIMU

0

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama kulia aliyesimama akizungumza na baadhi ya walimu mbali mbali, viongozi wa serikali, na  madiwani wakati wa halfa hiyo fupi ambayo ilianfdaliwa kwa ajili ya kuwapongeza walimu na shule ziliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

Baadhi ya walimu kutoka shule mbali mbali zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa wanafuatilia jambo kwa umakini wakati wa halfa hiyo ambayo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa  halmashauri hiyo.

*************************

NA VICTOR MASANGU, KISARAWE

WALIMU wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wametakiwa kuachana na tabia ya uzembe na badala yake wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa nidhamu  na weledi kwa lengo la  kutoa elimu bora  ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi katika kuongeza kiwango cha ufaulu na kufanya vizuri katika masomo yao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama wakati wa halfa fupi ambayo iliandaliwa maalumu kwa ajili ya kuwapongeza walimu na baadhi ya shule vizuri katika mitihani ya Taifa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, madiwani, wakuu wa idara pamoja na walimu kutoka shule mbali mbali.

Gama alisema kwamba wigo wa elimu ni mpana sana hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kwa walimu wenyewe pamoja na wanafunzi katika suala zima la kuwa na nidhamu pamoja na maadili na kuwaasa wanafunzi kuzingatia maelekezo na mafundisho mbali mbali ambayo wanapatiwa na wazazi na walezi pindi wanapokuwa nyumbani pamoja na mashuleni.

“Wazazi na walezi ni jukumu lenu kwa kushirikiana na walimu kuhakikisha kwamba mnasimamia nidhamu ya watoto wenu na kuhakikisha kwamba vijana wao wanafika shuleni bila kutegea na kwamba wanasoma kwa bidii hivyo katika hili ninawaomba sana mkalisimamie ili siku za usoni liweze kuleta matokeo chanya ya kuongeza kasi ya kufanya vizuri,”alifafanua Gama.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi aliwataka walimu kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya nidhamu kwa lengo la kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuboresha sekta ya elimu katika shule mbali mbali zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.

“Kwa kweli kwa upande wangu napenda  kuchukua fursa hii kuwaaagiza walimu wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na tena kwa weledi wa hali ya juu nia yetu ni kujenga misingi mizuri ya kuboresha sekta ya elimu katika shule zeto mbali mbali zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kwamba kitu kikubwa ni kuweka nidhamu ili kutimiza malengo waliyojiwekea,”alisema Mwanana.

Aidha Katibu Tawala huyo alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inawawekea mazingira rafiki kwa wanafunzi pamoja na walimu ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu sambamba na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya madarasa ili wanafunzi wasiweze kusoma katikahali ya mlundikano.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe aliwahimiza wazazi na walezi kuweka misingi imara ya kuhakikisha wanasimamia kwa umakini suala la  mwenendo wa watoto wao katika uwajibikaji wa kwenda shule pamoja na kuwahimiza wajitahidi kwa hali na mali waweze kusoma kwa bidii.

 Naye Diwani wa Kat ya Manerumango Hamisi Dipakutile alifafanua kwamba ili kutimiza azama y serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi inapaswa zifanyike juhudi za makusudi kwa walimu kuhakikisha wanaachana na tabia ya uzembe na badala yake waongeze bidii ya kufuwafundisha wanafunzi bila kutegea kwani baadhi yao wamekuwa ni wazembe.

“Ili jambo la elimu inapaswa kwa kweli litiliwe mkazo mno maana kuna baadhi ya shule kwa kipindi hiki cha mwaka wa 2012 hadi leo hii mwezi wan ne wamesoma topiki moja tu, nah ii inatokana na baadhi ya walimu wetu kutotekeleza majukumu yao ipasavyo kwa hivyo mimi naomba jambo hili liweze kufanyika kazi ili elimu yetu iweze kufika mbali zaidi na kufanya vizuri katika masomo yao,”alisema Dipakutile.

Abel Mudo ni Diwani wa kata ya Kisarawe naye alibainisha kuwa kumekuwepo na tabia ya wakuu wa shule kutotimiza wajibu wao ipasavyo na kupelekea hata walimu wengine kushindwa kufundisha kama inavyotakiwa hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa nia ya kuleta chachu ya elimu katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika sekta ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.