Home Mchanganyiko RC SHIGELLA AWATAKA WANANCHI WA MKOA WA TANGA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS SAMIA...

RC SHIGELLA AWATAKA WANANCHI WA MKOA WA TANGA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS SAMIA SULUHU

0

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa futari na kugawa msaada wa
vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal
kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa
iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima
la Taifa (NIC).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt
Elirehema Doriye akizungumza mara baada ya futari hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt
Elirehema Doriye katikati akigawa msaada  wa
vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal
kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa
iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima
la Taifa (NIC) kushoto ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt
Elirehema Doriye katikati akigawa msaada  wa
vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal
kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa
iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima
la Taifa (NIC) kushoto ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu

Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt
Elirehema Doriye katikati akipata futari sambamba na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tanga Judica Omari kushoto na Shehe wa Mkoa wa tanga Juma
Luwuchu kulia iliyaoandaliwa na Shirika hilo na kufanyika shule ya
Sekondari Jumuiya Jijini Tanga
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto aliyevaa suti nyeusi akiwa na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda wakipata futari ya
pamoja iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC)

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewataka wakazi wa
mkoa huo kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu na kumuunga mkono ili
anayotaka kufanya yawe makubwa zaidi kuliko kupindi cha miaka mitano
iliyopita.

Aliyasema hayo wakati wa futari na kugawa msaada wa
vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal
kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa
iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima
la Taifa (NIC).

Mkuu huyo wa Mkoa alisema serikali ni ya watu
wasikivu wana kiongozi hodari ambaye ni msikivu mwenye huruma lakini
ambaye hataki mambo ya mchezo na ambayo yanaweza kuwapoteza wananchi
Maendeleo.

“Tunapoomba dua kwa ajili ya Rais wetu Samia Suluhu
kwenye utendaji wake wa kazi nasi tujielekeze zaidi kwenye utendaji na
uwajibikaji kwa kutimiza majukumu yetu maana ya kazi iendelee na
alipojielekeza kwenye kazi iendelee maana yake juhudi kwenye ufanisi
zinahitajika kuongezeka zaidi”Alisema

“ Lakini tuendelee
kumuombea mwenyezi Mungu kwanza roho ya Marehemu Hayati John Magufuli
mwenyezi Mungu aipokee na aihifadhi mahali pema peponi pia tumuombee
Rais na kumuunga mkono ili aliyopanga kufanya yawe makubwa zaidi kuliko
kipindi cha miaka mitano iliyopita “Alisema

“Pia tunapokuwa
kwenye mfungo mtufuku tunamshukuru Rais Samia Sluhu yale maneno kuhusu
bomba la mafuta sasa linakuja Jumatatu wiki hii walikuja wataalamu wa
bomba la mafuta kueleza namna walivyofikia muda sio mrefu hatua ya
kwanza itakuwa ni kulipa fiidia kwenye eneo lote bomba
litakaopita”Alisema RC shigella.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema hatua
ya pili ni kulipa fidia kwenye maeneo yatakayogusia kwenye ujenzi
makambi na ujenzi wa Bandari Chongolea na ujenzi Matenki yakayatumika
kuhifadhi mafuta hayo ambayo yatakuwa yakitokea Hoima nchini Uganda hadi
Tanga.

Alisema miradi huo ni mikubwa na utengeneza ajira nyingi
na fursa za kibiashara kwa wananchi hivyo wao kama serikali
watahakikisha wanatenda haki kusimamia maslahi yao ambayo wanaweza
kusimamia kwenye mkoa ili wananchi wao wawze kunufaika.

“Lakini
kwa wale watakaopata biashara ya kusambaza mchanga,maji,chakula ,malori
ya mafuta itakapokuwa inahitaji kuwekeza bima tusuitafue bima nyengine
bali tuenda kwa Shirika la taiufa la Bima (NIC)”Alisema RC Shigella.

Awali
akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt
Elirehema Doriye alisema wameamua kuanza kuwafuturisha mkoa wa Tanga
na wamezingatia wenye mahitaji muhimu ikiwemo yatima wanaoishi kwenye
mazingira magumu.

Alisema ndio maana wameamua kupelekea bidhaa hizo zenye thamani ya milioni 4 kwa watoto watakaotumia msaada huo utawasaidia.

“Nimshukuru
sana Shehe wa Mkoa kwa kuendelea kujenga misingi ya ushirikiano na sisi
watumishi wa serikali kazi inakuwa nyepesi kwenye misingi ya umoja
unapokuwa na viongozi aina yako kazi ytu inakuwa nyepesi”Alisema

Mkurugenzi
huyo alisema wamejumuika na waislamu katika mkoa wa Tanga kwa ajili ya
kufuturisha watoto yatima na waislamu mwenye mwezi huu wa Ramadhani
ikiwa ni sehemu mojawapo ya kurudisha kwa jamii .

“Kama sehemu
ya jamii tunajumuika na jamii imekuwa ikiwatusapoti kwenye shughuli zetu
na kuwasaidia wale ambao hawajapata bahati ya kuishi maisha
wanayoiyategemea watoto yatima ambao hawana wazazi na wanahitaji misada
ya kijamii”Alisema

Alisema msaada huo ni sehemu ya kuonyesha
mshikamano wao kwa jamii ya waislamu ikiwemo kutekeleza baadhi ya
maelekezo ya Rais Samia Suluhu ambapo kwenye kongamano la Viongozi wa
dini alisema wanahitaji kushirikiana kwa pamoja kuwa na umoja na kujenga
jamii bora.

Alisema pamoja na kufuturu nao lakini wametoa
msaada kwa ajili ya watoto yatima Tanga ni mkoa wa Tanga na wataendelea
kwenye mikoa mingine.

“Tunaheshimu ibada ambayo inaendelea ni
pamoja na Sukari,Tende,Sabuni pamoja na mafuta na vitu vyote ambavyo
vinaweza kuwasaidia kwenye mwezi wenye thamani ya milioni 4 na
tutaendelea kutoa kwenye mikoa mingine”Alisema