Home Michezo SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR MABAO 2-0 KWENYE UWANJA WA KAITABA

SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR MABAO 2-0 KWENYE UWANJA WA KAITABA

0

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba Sc leo imeendelea kuvuna pointi baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0 kwenye uwanja wa Kaitaba.

Mabao yote mawili yamepatikana katika kipindi cha kwanza kwani kipindi cha pili timu zote zilikuwa ngumu kuruhusu nyavu zao kutikiswa.

Mabao ya Simba yaliwekwa kimyani na nyota wao Luis Miquissone dakika ya 13 ya mchezo baadae mshambuliaji Chris Mugalu alifunga hesabu za mabao kwa kupachika bao dakika 24.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 55 ikiawa tofauti ya pointi mbili na watani wa jadi Yanga wenye pointi 57.