Home Michezo KMC FC KUSHUKA TENA DIMBANI DHIDI YA BIASHARA KESHO

KMC FC KUSHUKA TENA DIMBANI DHIDI YA BIASHARA KESHO

0

********************************

Mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Gwambina, kikosi cha KMC kesho kitakuwa katika mchezo mwingine dhidi ya Biashara utakaopigwa saa 14:00 mchana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

KMC FC ambao watakuwa ni wenyeji katika mchezo huo dhidi ya Biashara inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya goli moja kwa moja ikiwa ugenini katika uwanja wa CCM Karume Musoma Mkoani Mara timu hizo mbili zilipokutana katika Duru ya kwanza.

Aidha katika mchezo kesho KMC FC inahitaji ushindi iliiweze kuendelea kujiimarisha zaidi katika nafasi za msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania na hivyo kufikia malego ambayo kama Timu ilijiwekea ya kumaliza Ligi ikiwa kwenye nafasi nzuri.

Licha ya kwamba katika mchezo huo kutakuwa na upinzani mkubwa lakini bado tunaimani na kikosi kilichopo kutokana na maelekezo ambayo walimu Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wachezaji hao.

KMC FC inahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili kuiwezesha Timu kupanda katika nafasi Nne za juu ambayo kwa hivi sasa inashikiliwa na Timu ya Biashara.

“ Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi tunafahamu kabisa utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu ambayo tunakutana nayo, wanafanya vizuri, lakini pia wako kwenye nafasi ya Nne hivyo tumejipanga kuingia kwenye mchezo huo pasikuwa na hofu.

Hadi sasa Timu ya KMC ipo katika nafasi ya tano na kwamba katika mchezo uliopita dhidi ya gwambina, iliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri, ambayo yalifungwa na Charles Ilamfya, Ally Ramadhani pamoja na Emmanuel Mvuyekule.

Imetolewa leo Aprili 19

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC FC