……………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha stendi kuu ya Mabasi iliyopo Katumba Azimio katika Manispaa hiyo kuwa inafunguliwa ifikapo tarehe 15.5.2021
Mh. Wangabo amesema kuwa awali Mkurugenzi huyo alitaka kuifungua stendi hiyo mwezi 29.1.2021 na kushindikana baada ya baadhi ya miundombinu kutokamilika vizuri na hivyo kuwaopa wiki moja kurekebisha miundombinu hiyo ndipo waifungue stendi hiyo tarehe 5.2.2021 na matokeo yake stendi hiyo haijafunguliwa hadi mwezi huu Aprili.
“Mpaka tarehe 15.5.2021 uwe umekamilisha kwa maana, ninyi ndio mliotaka kufungua siku moja kabla ya siku ile mi kufika (28.1.2021) halafu leo kuanzia mwezi ule wa pili, wa tatau, wa nne, unaongeza tena mwezi mwingine, imetoka wapi? Mkurugenzi fanya juu chini tarehe 15.5.2021 iwe mwisho, tunahitaji mapato pia, wananchi hawa wameeleza kero nyingi hapa zinahitaji fedha na fedha hizi zinatakiwa zitoke halmashauri sio kwa Mkuu wa mkoa,” Alisisitiza.
Mh. Wangabo alisema hayo (14.5.2021) katika hafla fupi ya kukabidhi hati kwa wananchi 13 wa Mtaa wa Sokolo baada ya zoezi la urasimishaji makazi katika mtaa huo kuisha na kuongeza kuwa kuwa ili changamoto za wananchi zitatuliwe halmashauri zinatakiwe zikusanye pesa kwa wingi na kutatua changamoto hizo na stendi hiyo ikikamilika ina uwezo wa kukusanaya karibu shilingi bilioni moja na hivyo kurahisisha mahitaji ya wananchi
Aidha katika hatua Nyingine Mtendaji mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya alipotembelea katika stendi hiyo tarehe 15.4.2021 katika ziara yake ya kutembelea miradi ya kimkakati iliyopo Manispaa ya Sumbawanga alisema kuwa ni vyema Manispaa hiyo ikazingatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ili kuongeza mapato katika halmashauri.
“mkurugenzi ameniambia kwamba utayari wa wamiliki wa mabasi uko juu sana, wako tayari kuja wakati wowote hapa, kama alivyotoa maelekezo mkuu wa mkoa, kufikia tarehe 15.5.2021 wajitahidi kukamilisha ili kuhakikisha stendi hii inafanya kazi ili kukidhi madhumuni ya stendi hiyo ambayo ni kupunguza msongamano mjini pamoja na mapato, mimi nakijita kwenye mapato kwasababu ndio lengo kubwa, tupate mapato ambayo yatatusaidia kutoa huduma kwa wananchi,” Alisema.
Mapaka tarehe 15.4.2021 stendi hiyo imeshakamilika kwa asilimia 92 na kubakisha maeneo machache ikiwemo vibanda vya mama lishe na wafanayabiashara ambavyo vinaweza kuendelea kumaliziwa wakati stendi hiyo ikiendelea kufanya kazi.