Home Biashara WAKULIMA WA ZAO LA MUHOGO MKOANI PWANI WAASWA KUTUMIA KILIMO CHA KISASA-RC...

WAKULIMA WA ZAO LA MUHOGO MKOANI PWANI WAASWA KUTUMIA KILIMO CHA KISASA-RC NDIKILO

0
………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAKULIMA wa mhogo mkoa wa Pwani ,bado hawajanufaika zaidi na zao hilo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na soko la uhakika na baadhi yao kutotumia mbegu bora na kilimo cha kisasa.
Pia uwekezaji mdogo katika kilimo cha muhogo ,mkoa bado haujapata wawekezaji wakubwa kwa maana ya kulima ,na kujenga viwanda vikubwa vya kusindika muhogo.
Akifungua mkutano wa wadau wa zao la muhogo mkoa,mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema, mazao makuu ya chakula mkoani humo, ni muhogo ,mpunga,mahindi,viazi vitamu,mtama,ndizi na jamii ya mikunde ambapo muhogo ndilo linaloongozwa kulimwa kama zao la chakula na biashara.
Alisema,zao hilo linachukua eneo la wastani wa hekta 60,703 kwa mwaka na kwa sehemu kubwa kinahusisha wakulima wadogo wanaolima kati ya ekari 0.5-2 kwa mwaka.
Ndikilo alibainisha, hekta 60,703 ni sawa na asilimia 3.1 zinalimwa tani 500,000 eneo hilo ni dogo kwa uzalishaji kwani eneo lililopo ni hekta milioni 1.9 .
“Halmashauri zilizokinara kwa kulima muhogo ni Rufiji,Kibiti,Mkuranga,Kisarawe na Kibaha ambapo tani 20 uzalishwa kwa hekta moja ,lakini kutokana na changamoto zilizopo wakulima hawa hawafikii malengo ,soko halijaleta tija na hawana fedha za kutosha ” alifafanua Ndikilo.
Ofisa kilimo wa mkoa , Specioza Kashangaki alizihimiza halmashauri kuanzisha vituo vya kukusanyia na kuuzia muhogo pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara zinazokwenda maeneo ya uzalishaji ili kuvutia wanunuzi na wasafirishaji.
Kashangaki aliwataka wakulima, kutumia mbegu bora ,kufuata kanuni bora za kilimo na kuongeza maeneo yanayolimwa.
Nae mwenyekiti wa TACAPPA ,Mwantumu Mahiza ,alifafanua kufikia soko la Uchina haiwezi kuwa suluhisho badala yake vijengwe viwanda vya kusindika muhogo.
Mahiza aliwaasa wakulima kuachana na jembe la mkono na kutumia kilimo cha kisasa ,kwani katika heka moja unaweza kupanda vijiti 4,000 na shina moja likauzwa kwa sh.1,000 jumla milioni NNE .