Home Michezo KMC KUKUTANA NA GWAMBINA KESHO UWANJA WA UHURU

KMC KUKUTANA NA GWAMBINA KESHO UWANJA WA UHURU

0

Mara baada ya kutoka sare dhidi ya Yanga, Kikosi cha KMC FC hapo kesho kitakuwa tena katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Gwambina saa Kumi Jioni.

KMC FC itakuwa mwenyeji katika mchezo huo na hadi sasa Timu imeshafanya maandalizi ya kutosha na hivyo ipo tayari kwa mtanange huo.

Kikosi hicho cha wana Kino Boys kinachonolewa na Makocha John Simkoko kocha Mkuu pamoja na Habibu Kondo Kocha Msaidizi kinaingia uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya kushinda dhidi ya Gwambina ugenini Misungwi mkoani Mwanza ambapo KMC iliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri.

Hali ya kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni iko vizuri na itakosa huduma ya wachezaji watatu wenye majeraha ambao ni David Brayson, Kenny Ally Mwambungu pamoja na Sudi Dondola na wachezaji wengie wote wako vizuri.

“Tunafahamu kwamba tunakwenda kukutana na Timu ambayo ilipata ushindi wa magoli manne kwa sifuri dhidi Coast, lakini ushindi huo kwetu hautupi wasiwasi na tunachokiamini ni kwamba KMC tumefanya maandalizi mazuri kwa mchezo wa kesho na tuna imani yakupata matokeo mazuri.

Aidha tumetoka kutoa sare dhidi ya Yanga sasa nguvu zetu tunazielekeza tena katika mchezo wa kesho ambao kimsingi ni muhimu lakini pia una ushindani mkubwa ila kikubwa ni kwamba tunapambania kama timu kupata alama tatu.