Home Mchanganyiko Wizara mbili zatekeleza maelekezo ya Rais

Wizara mbili zatekeleza maelekezo ya Rais

0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul (kushoto) akizungumza leo katika kikao cha Mawaziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na  Wizara hiyo cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma, anayefuata ni Waziri wake Innocent Bashungwa akifuatiwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na kulia ni Naibu wake Mhandisi Kundo Mathew. Kikao  hicho  kimefanyika  kufuatia  maelekezo  yaliyotolewa  hivi karibuni na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kutaka  kufanyika  marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombo vya Habari  hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)

Wajumbe wa kikao cha Mawaziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika kikao hicho cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kikao  hicho  kimefanyika  kufuatia  maelekezo  yaliyotolewa  hivi karibuni na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kutaka  kufanyika  marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombo vya Habari  hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas (kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akifuatiwa na Naibu wake Dkt. Jim Yonaz katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo mbili cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kikao  hicho  kimefanyika  kufuatia  maelekezo  yaliyotolewa  hivi karibuni na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kutaka  kufanyika  marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombo vya Habari  hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas (kushoto) akizungumza leo katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hiyo na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula. Kikao  hicho  kimefanyika  kufuatia  maelekezo  yaliyotolewa  hivi karibuni na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kutaka  kufanyika  marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombo vya Habari  hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)

***************************

Na John Mapepele, Dodoma

Waziri anayesimamia Sekta ya Habari Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri anayesimamia Sekta ya Mawasiliano Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na timu ya Makatibu  Wakuu na Wataalam  wa Wizara hizo  wamekaa na kujadili  hoja mbalimbali kuhusu  utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za kisekta kufuatia  maelekezo  ya hivi karibuni ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maelekezo hayo aliyatoa   wakati wa  kuwaapisha Makatibu Wakuu, Naibu  Makatibu  Wakuu na  Wakuu wa Taasisi ya kufanya marekebisho ya Sheria na Kanuni  zinazosimamia Vyombo vya Habari hususan Televisheni Mtandao (Online TV).

Majadiliano hayo yamefanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2021 na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwenye hoja 13 zilizoainishwa na Wizara hizo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa  amesema miongoni mwa  maazimio  yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya  mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo katika maeneo yote yenye mapungufu  ili ziendane na  hali halisi ya sasa  na  kuweka  mifumo rafiki ya kushughulikia masuala  yote  yanayohusu sekta ya  Mawasiliano na Utangazaji

“Tumeagiza Wataalam wafanye uchambuzi wa Kanuni za Maudhui Mtandaoni ili kuona kama zinaendana na mazingira ya sasa” amesisitiza Waziri Bashungwa

Ameongeza kuwa Wizara zimeaazimia kuja na mkakati wa kuwaelimisha  wadau wa Sekta hizo ili kudhibiti makosa  ya kimaudhui  yanayofanywa  na Vyombo vya Habari badala ya hali ilivyo sasa inayotoa adhabu kali zinazojikita kwenye utozaji wa faini kubwa pamoja na kufungiwa.

Suala lingine ambalo limeazimiwa kufanyiwa kazi ni chaneli za bure kutoonekana kwenye visimbusi ambavyo kimsingi zinapaswa kuonekana hata pale kifurushi kinapokuwa kimeisha muda wake.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine  Ndugulile amesema kukua kwa teknolojia kumewezesha kukua kwa matumizi ya huduma za mawasiliano yakiwemo ya utangazaji hivyo katika kipindi kifupi  kijacho Serikali  kupitia  Wizara hizo mbili  itafanya  maboresho  makubwa  kwenye kanuni husika ili kuendana na  hali halisi ya sasa.

Ameongeza kuwa Serikali ilitunga Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali zikiwemo Sheria ya huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 ambazo pamoja na mambo mengine zinaelekeza kuweka mazingira wezeshi ya kukuza maudhui ya ndani (Local content)