Home Michezo SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR MABAO 5-0, YATEMBEZA PIRA BIRIANI

SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR MABAO 5-0, YATEMBEZA PIRA BIRIANI

0

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba Sc imeifulumishia mvua ya magoli klabu ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo imeichapa magoli 5-0 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc imecheza mchezo huo baada ya kutoka kucheza mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika,

Magoli ya Simba yaliyewekwa kimyani na Clatous Chota Chama ambaye alifungua hesabu ya magoli mnamo dakika ya 9 ya mchezo kabla ya Rally Bwalya kufunga bao la pili dakika ya 19 na baadae Meddie Kagere akafunga bao la tatu.

Timu zilikwenda mapumziko wakati Simba ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Simba iliendelea kulisakama lango la Mtibwa Sugar licha ya kukosa mabao mengi walifanikiwa kupata bao la nne kupitia kwa Medie Kagere dakika ya 51 na baadae Louis Miquisone.