Home Mchanganyiko MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA MWENYEJI WAKE RAIS MUSEVENI WA UGANDA...

MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA MWENYEJI WAKE RAIS MUSEVENI WA UGANDA WASHUHUDIA UTIWAJI SAINI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MMASHARIKI IKULU YA ENTEBBE LEO

0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akiweka saini kwenye kitabu cha ratiba ya hafla  ya uwekwaji saini wa
mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka
Hoima nchini Uganda hadi Tanga baada ya yeye na Rais Yoweri Museveni
wa Uganda kuombwa na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya Total
duniani Bw. Patrick Poyanne kufanya hivyo ili iwe kumbukumbu yake ya
siku hiyo ya kihistoria katika Ikulu ya Entebbe leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akiweka saini kwenye kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na mwenyeji
wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe
mchache kabla viongozi hao kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa
ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt.James Mataragio akiweka saini kwa niaba ya Tanzania mkataba wa ujenzi
wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda

Maafisa wandamizi wa kampuni ya TOTAL ya Ufaransa  wakiweka saini
mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka
Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya
Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan akisindikizwa na  mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda katika Ikulu ya Entebbe baada ya  hafla ya uwekwaji saini wa
mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka
Hoima nchini humo hadi Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
wakipata picha ya kumbukumbu na  mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta
Museveni wa Uganda na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya
TOTAl duniani Bw. Patrick Pouyanner na viongozi waandamizi wa bn hi
hizo mbili na kampuni hiyoa katika Ikulu ya Entebbe baada ya  hafla ya
uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika
Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga.