Home Mchanganyiko TAFITI ZICHANGIE KUZAA SERA NA MAENDELEO YA NCHI

TAFITI ZICHANGIE KUZAA SERA NA MAENDELEO YA NCHI

0

Mratibu wa Utafiti na machapisho katika Kurugenzi ya Shajada za Uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu SUA Prof. Japhet Kashaigili wakati akifunga hafla fupi ya kufunga mradi wa kuwezesha matokeo ya tafiti ili kuzaa sera iliyofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mhalangu ya sayansi na Elimu.

Mkuu wa idara ya Mipango,Sera na Utawala ya Ndaki ya Sayansi ya jamii na humanitia Prof. Fatihia Massawe akifungua hafla hiyo.

Mkuu wa Mradi huo Dkt. Faith Mabiki akizungumza wakati wa hafla hiyo juu ya  malengo ya hafla hiyo namradi pamoja na mafanikio yaliyopatikana. 

Dkt. Onesmo Nyinondi akichangia jambo wakati wa hafla hiyo.

Wadau wote wa mradi na wageni waalikwa walioshiriki kwenye hafla hiyo wakifuatilia malezo ya mradi na michango ya washiriki kwenye mradi huo.

Wadau wote wa mradi na wageni waalikwa walioshiriki kwenye hafla hiyo wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.

Wadau wote wa mradi na wageni waalikwa walioshiriki kwenye hafla hiyo wakifuatilia malezo ya mradi na michango ya washiriki kwenye mradi huo.

Mlezi mshauri wa mradi huo Prof. Lusato Kurwijila akizungumza naneo wakati wa hafla hiyo ya kuhitimisha mradi huo.

*****************************************

8/4/2021                        Morogoro                               Matokeo

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wameshauriwa kuhakikisha wanaweka fedha kwaajili ya kusambaza matokeo ya utafiti kwa walengwa na kuchangia katika kutengeneza sera au kuziboresha wanapoandika maandiko ya miradi yao kwa wafadhili.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Utafiti na machapisho katika Kurugenzi ya Shajada za Uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu SUA Prof. Japhet Kashaigili wakati akifunga hafla fupi ya kufunga mradi wa kuwezesha matokeo ya tafiti ili kuzaa sera iliyofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mhalangu ya sayansi na Elimu.

Prof. Kashaigili amesema kumekuwa na tafiti nyingi nzuri ambazo zinafanywa na Watafiti wa SUA lakini bado mchango wake haujaonekana sana katika kusaidia utungaji wa sera na uboreshaji wa sera zilizopo na matokeo yake zinatumika kwenye kuwapatia watafiti shahada na kupanda madaraja.

‘’ Ukiangalia hata swala la usambazaji wa matokeo ya tafiti zetu mara nyingi tunaweka hela kidogo sana na muda mwingine hatuweki kabisa kwenye baadhi ya miradi ninayoifahamu lakini hili linafanyika bila kujua kuwa uchakataji wa matokeo ya utafiti husika ili kupata sera ni sehemu  ya usambazaji wa matokeo kwa walengwa  na kutokuweka bajeti maana yeke huna kitu cha kusambaza’’ Alisema Prof. Kashaigili.

Ameongeza kuwa kwa sasa kuna ulazima kwa kila mtafiti kuweza kujua mbinu muhimu kabisa za namna ya kuandika matokeo hayo kwa walengwa wa utafiti kwa kuandika kifupi lakini kwa kutumia lugha inayoweza kueleweka kirahisi na kufikisha ujumbe kirahisi kwa sababu wengi hawajua kinachofanyika chuoni hapo.

Prof. Kashaigili amepongeza uongozi wa mradi huo kwa kuamua kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Chuoni hapo kuwaeleza malengo ya mradi na matokeo yake na hivyo na kusaidia hata watafiti wengine kuona kilichofanyika na kusema kuwa huu kitendo hiki kiigwe na watafiti wengine chuoni hapo kuhabarishana yake yanayofanywa na watafiti wengine chuoni.

Awali akifungua hafla hiyo Mkuu wa idara ya Mipango,Sera na Utawala ya Ndaki ya Sayansi ya jamii na humanitia Prof. Fatihia Massawe amesema ili kuhakikisha kile watafiti wanafanya kinazaa sera wasitegemee utafiti mmoja pekee maana hauwezi kumshawishi mtunga sera kutengeneza sera bali zifanyike tefiti nyingi kwenye mitazamo tofauti kama vile Uchumi, Kijamii na hata kiafya.

‘’Ili tuweze kupeleka andiko letu la kusaidia kuzaa sera lazima tuhakikishe limeshiba kwa maana limegusa kila eneo kwa mapana yake kwani kuna taarifa nyingine zinazobeba andiko lako la sera la sivyo tutaendelea kubaki hapa tulipo sasa tukitaka kila utafiti na kila mradi uzae sera’’ Alisisitiza Prof. Fatihia.

Amesema uanzishwaji wa kituo hicho cha kimataifa cha kuchakata matokeo ya butafiti ili kuzaa sera kutasaidia sana katika kuunganisha nguvu na uwezokwa pamoja katika kufanya tafiti kwa upana zaidi na kuchangia kwenye utungaji wa sera mbalimbali za nchi.

Akizungumzia malengo ya mradi huo wa miezi sita Mkuu wa Mradi Dkt. Faith Mabiki amesema malengo ya hafla hiyo ilikuwa ni kuwaktanisha wadau wote chuoni hapo kujua nini walikuwa wanafanya kwani kumekuwa na tafiti nyingi zinafanyika chuoni hapo lakini mtafiti mmoja hajui mtafiti mwingine anafanya nini na amepata matokeo gani.

Amesema kuwa malengo ya mradi huo ilikuwa ni kutaka kuona kama watafiti wanaweza kuchangia kwenye kuzalisha sera za nchi au kuboresha sera zilizopo ili kupata sera nzuri kutokana na utafiti,kujenga uelewa miongoni mwa watafiti  na watunga sera kuona umuhimu kutumia matokeo ya utafiti  kuzalisha serana  kujenga uwezo kwa watafiti katika kuandika matokeo yao kwa lugha nyepesi na kuaizisha kituo cha kuchakata matokeo ya utafiti SUA ambacho kitasaidia kukusanya tafiti zote ndani nan je ya nchi ili zisaidie kutumiwa kuzalisha sera.

Dkt. Mabiki amempongeza Makamu mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda kwa mchango wake mkubwa kwenye utekelezaji wa malengo ya mradi huo hasa wakati wa uandaaji wa mdahalo ambao ulifanyika mwaka jana na kuwa na matokeo makubwa ambayo sasa yanakwenda kuzaa kituo hicho kikubwa nchini.