Home Mchanganyiko WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWAKUANZA VYEMA NA KUKUBALIKA NA WATANZANIA

WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWAKUANZA VYEMA NA KUKUBALIKA NA WATANZANIA

0

Mwekezaji wa shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY zilizopo mwanza ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Ezekiel Mollel akiongea 

…………………………………………………………………………………….

Na Woinde Shizza,  ARUSHA 

Uongozi shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY umempongeza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Samia Suluhu kwa kuanza vizuri kazi yake na kukubalika na makundi yote katika jamii ya watanzania.
Pongezi hizo zimetolewa na muwekezaji wa shule hizo ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Mwl.Ezekiel Eliphas Meivule Mollel ambapo alimuahidi Rais Samia kumpa ushirikiano wa asilimia zote katika sekta ya elimu.
Aidha pia alisema kasi aliyoingia nayo Rais Samia ni nzuri na anauhakika kabisa itaweza kuivusha nchi ya Tanzania , na kuwafikisha watanzania mbali zaidi katika swala la Maendeleo ukizingatia nchi yetu ina vitega uchumi vingi.
 Aliongeza kuwa wataendelea kumuweka katika maombi yeye na viongozi wenzake wa serikali ili waweze kuyatekeleza yale yote ambayo amekusudia kuwafanyia watanzania ikiwemo kumaliza miradi yote mikubwa iliyoachwa na hayati John Magufuli pamoja na kuwaletea maendeleo ya nchi pamoja na mtu mmoja mmoja.
 Alisema wanaona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi pamoja na kusaidia katika kuleta Maendeleo ya nchi .
Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuongeza ajira kwa walimu 6000 ambao wapo mtaani na kusema kuwa hii itadaidia kuboresha elimu yetu iendelee kuwa bora zaidi,pia alipongeza mikakati mipya aliyoitagaza ikiwemo kuhamasisha uchimbaji wa madini 
Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza wakafanya mambo yakaenda sawa.
Alibainisha kuwa jamii yenye ufahamu wa kutosha juu ya wajibu wake katika utawala bora, demokrasia na haki za binadamu, ni jamii inayowajibika na inayoshiriki 
kikamilifu, na kwa hiari katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa taifa.