Home Mchanganyiko KAMPUNI YA XING J.X YATOA MSAADA KWA YATIMA

KAMPUNI YA XING J.X YATOA MSAADA KWA YATIMA

0

MKURUGENZI na mfanyabiashara wa Kampuni ya Xing J.X ya China, Xheng Jian, akimkabidhi Katibu wa Kituo cha Kulea Yatima cha Malaika, Khadija Said,msaada wa bidhaa mbalimbali,Kinondoni, Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Mfadhili wa kituo hicho, Juma Gurumo.

*******************************

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Xing J.X ya China, imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulea Yatima cha Malaika, kilichopo Kinondoni, Vijana, Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi MKuu wa kampuni hiyo Xheng Jian, ya China, alisema, dhamira ni kusaidia jamii kwa kutoa gawio la faida hasa kwa jamii ya watu wenye mahitaji maalumu.

Jian alisema, kampuni hiyo inatambua dhima ya uwekezaji hapa nchini hivyo inawajibu mkubwa wa kurejesha faida kwa wananchi hasa watu wenye mahita.

ji maalumu.

“Pia msaada huu ni kuunga mkono jitihada za kusaidia watu wenye mahitaji maalumu alio kuwa akihimiza Hayati Rais Dk. John Magufuli. Tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kurejesha faida tunazo pata katika biashara zetu kwa jamii,”alisema.

Mfadhili wa Kituo cha Malaika, Juma Gurumo, aliishukuru kampuni hiyo ya Xhing J.X, kwa msaada huo.

“Wamekabidhi mchele, mafuta ya kupikia, sukari, mifuko mbadala, sabuni, unga wa sembe na dawa za kusafishia maliwatoni. Tunawashukuru sana,”alisema Gurumo.

Alisema, Xhing J.X licha ya kuwa ni kampuni ya kigeni kutoka china iliyowekeza nchini ukiwemo uwekezaji mkubwa katika michezo ya kubashiri au Kubeti imetambua jukumu la kusaidia kada ya yatima hivyo kuzitaka kampuni zingine na wadau kuiga mfano huo.

Katibu wa Kituo cha Malaika, Khadija Said, alishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo ambao alisema utahudumia watoto zaidi ya 300 wanaolelewa na vituo vya Malaika.