Home Mchanganyiko WAZIRI DK.MWIGULU ATAKA WATENDAJI WENYE JUKUMU LA KUKUSANYA KODI KUFUATA SHERIA YA...

WAZIRI DK.MWIGULU ATAKA WATENDAJI WENYE JUKUMU LA KUKUSANYA KODI KUFUATA SHERIA YA UKUSANYAJI MAPATO NCHINI

0

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba,akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa kikao cha Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA) kilichofanyika leo April 3,2021 Jijini Dodoma.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba,akisisitiza jambo  wakati wa kikao cha Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA) kilichofanyika leo April 3,2021 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa kikao cha Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA) kilichofanyika leo April 3,2021 Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga,akizungumza wakati wa kikao cha Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA) kilichofanyika leo April 3,2021 Jijini Dodoma.

Baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba, wakati wa kikao cha Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA) kilichofanyika leo April 3,2021 Jijini Dodoma.

………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amekutana na watalaamu wa wizara hiyo na kuwataka watendaji wenye jukumu la kukusanya kodi kuhakikisha wanakusanya kodi kwa wafanyabiasha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwa kuchukua kiasi cha kodi kinachohitajika  na si kuua shughuli ama biashara kwa kuchukua fedha zisizostahili.

Akizungumza na wandishi wa habari leo April 3,2021 jijini Dodoma.Dk Nchemba amewataka watumishi wa wizara hiyo na mamlaka zinazosimamia ukusanyaji wa mapato kurekebisha pale walipokosea ikiwa ni pamoja na kurudi kwenye mstari kwa kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria wakizingatia weledi wa kazi yao.

Waziri Nchemba amesema kuwa  ni wakati sasa wa kulinda uchumi wa Taifa letu kwa kuwalinda pia walipa kodi huku akiwataka wafanyabiashara ambao walikua wanaogopa kuweka wazi fedha zao waweke kwenye mabenki kwani serikali itatoza kodi inayostahili na siyo kuchukua fedha za watu.

“Wizara lazima jambo hili ilifanyie kazi kwa kina na kulitekeleza kikamilifu,  lazima tukuze uchumi wetu, tulinde walipa kodi waliopo, tutengeneze walipa kodi wapya, tuwalinde na si kuwaua walipa kodi na kutanua wigo,”amesema

Dk.Nchemba amesema kuwa kila Idara na Taasisi iliyoko chini ya wizara yangu lazima ilipe jambo hilo kipaumbele hakikisheni mnarudi kwenye mstari kwa kuangalia ni eneo gani tulikosea na kuua shughuli za wafanyabiashara ili waanze upya kwa kutumia misingi inayowaongoza.

“Mlipa kodi amekadiliwa, kukaguliwa na kupewa cheti na mwaka hadi mwaka, akiwa amejua yameisha na anaendelea na shughuli zake, ghafla anaambiwa lete taarifa ya miaka 10, si sawa kwanza kwa utamaduni wetu hakuna mtanzania anayeweza kuhifadhi lisiti kwa muda mrefu kiasi hicho,tunawachanganya wlipa kodi,”amesisitiza

Waziri Nchemba amewataka watendaji kutoka huko kwenye kuwakadilia kodi ,wakadilie kodi kwa  kumjibu wa sheria zao wasifanye kinyume cha sheria na taratibu husika, muwe na weledi katika kukusanya kodimana tunayomiongozo inayotuongoza katika utekelezaji wa majukumu hayo na wizara itaendelea kuwafuatilia

Dk.Nchemba amesema kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa mapato kama walivyoelekezwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kufuata sheria na taratibu za ukusanyaji wa mapato bila kuathiri uchumi wa Nchi na wa walipa kodi.

Aidha Dk.Nchemba ametoa onyo kwa walipa kodi ambao wamekuwa na janja janja ya kulipa kodi kuacha tabia hiyo mara moja, mana kukwepa kodi ni kuvunja sheria na ni jambo ambalo halivumiliki kwa kwa serikali hii.

Waziri Nchemb amesema kuwa ni lazima kila mlipa kodi ajenge tabia ya kulipa kodi kwa hiari na si kukwepa kodi, wazingatie taratibu, mifumo ya ulipaji wa kodi iliyopo na maelekezo yanayotolewa na serikali.

Hata hivyo amesema kuwa Pia Serikali inatarajia kuangalia mifumo iliyo bora zaidi katika ukusanyaji wa kodi nchini ambayo itawezesha mlipa kodi kubaini namna kodi yake inavyofanya kazi,  lengo ni kuchochea wananchi kulipa wakitambua fedha yao inapokwenda.

Naye Kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamadi Masauni amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwateua yeye na Dk Nchemba katika nafasi hizo huku wakiahidi kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kama ambavyo ameelekeza.

”Sisi kama Wizara tumepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Rais, Samia na tutahakikisha tunayafanyia kazi kikamilifu ili nchi iweze kusonga mbele, kukuza uchumi na kujiletea maendeleo”amesema Mhandisi Masauni