Home Mchanganyiko RC NDIKILO AKEMEA BAADHI YA HALMASHAURI KUDOKOA ASILIMIA 10 ZA MAKUNDI YA...

RC NDIKILO AKEMEA BAADHI YA HALMASHAURI KUDOKOA ASILIMIA 10 ZA MAKUNDI YA VIJANA ,WANAWAKE NA WALEMAVU

0

***************************************
2,april
Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo, amekemea baadhi ya halmashauri kutumia zinazotengwa kwa ajili ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya mikopo ya kundi la walemavu,wanawake na vijana na kuzitaka ziendelee kutenga fedha hizo ili kunufaisha vikundi hivyo.
Alitoa rai hiyo ,katika makabidhiano ya Vifaa na Fedha Taslimu vyenye thamani ya Sh.milioni 245,867,100 kama Mikopo  ya Asilimia10 ya Mapato ya Halmashauri ya Mji Kibaha kwa makundi ya Vijana, Wanawake  na Watu wenye  Walemavu.
Pia mkuu huyo wa mkoa ,amekabidhi Pikipiki 12, Bajaji 1, Toyo 1 Mashine 1 ya kutengeneza sabuni na Fedha taslimu sh.177,746,400 kwa vikundi 68.
Ndikilo alisema utoaji wa mikopo hiyo ni takwa  kisheria  (Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019),na ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Cha Mapinduzi 2020-2025.  
Akieleza  hali ya utoaji mikopo hiyo na marejesho Mkoani hapo alisema mwaka 2019/20 Jumla ya Shilingi  Bilioni 2.666  zilitolewa kwa vikundi 672 sawa na Asilimia 108 ya fedha zilizopangwa kutolewa na marejesho yalikuwa Sh. 645,770,927 sawa na asilimia 54 ya fedha zilizokopeshwa.
 “Marejesho haya ni Duni”  fedha hizi ni za Serikali lazima mrejeshe ili watanzania wengine wanufaike  na matunda ya  Serikali yao”
Ndikilo alisema kwa mwaka 2020/21 fedha za asilimia 10 zitakazotengwa   na Halmashauri zote 9  ni Bilion 2,124,500,000  hadi Februari 2021 fedha zilizokusanywa   ni Bilioni 1,713,172,068 sawa na asilimia 78.54 ya fedha zilizopangwa, fedha ambazo zimefikishwa kwenye vikundi hadi Februari 2021 ni Sh. Bn 1,149,459,447 sawa na asilimia 66.92.
Nawataka kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na vifaa wanavyokabidhiwa, “Hakuna fedha ndogo lazima muwe na mipango  thabiti ili fedha ziongezeke” alisema Ndikilo.
Nae mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Jeniffer Omolo ,alieleza kwa mwaka 2020/2021 vimeundwa vikundi 254 katika kata zote 14 za halmashauri hiyo.
Omolo alifafanua,Utoaji wa mikopo ,wanatenga fedha asilimia 10 kwa kufuata sheria ambapo wametoa milioni 83 mwaka 2017 /2018,na milioni 161 kwa 2018/2019 pia milioni 276 kwa mwaka 2019/2020 na milioni 373 kwa mwaka huu.